Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Joshua Nassari akanusha kufyatua risasi kwenye uchaguzi wa madiwani Daraja II Arusha jana

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari amekanusha taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari Leo kuwa jana alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha, uchaguzi uliofanyika jana ambapo mgombea wa Chadema aliibuka mshindi.

Nassari ameyasema hayo leo jioni wakati akihutubia katika Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na watu wengi, umefanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River ambapo mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ng Henry Kileo nae alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.

Nassari amedai kuwa katika uchaguzi wa jana yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya Bangata, iliyoko Arumeru Magahribi na hivyo kumhusisha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimkamata na kuandika maelezo yake kituoni, lakini anashangaa kuambiwa ni yeye wakati siyo!

Akifafanua zaidi aliviomba vyombo vya usalama avinavyohusika na maswala ya vibali vya kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze hiyo bunduki walimpa lini na ni risasi ngapi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata yeye yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.

DSCN5926Mh Nassari akihutubia mkutanoni hapo hii leo

DSCN5946Sehemu ya umati ulijitokeza katika ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Ngaresero, Usa-River

DSCN5906Katibu wa CHADEMA Kinondoni, Dar es Salaam, Henry Kileo akizungumza na wananchi wa Usa River leo jioni.Nassari alisema kampeni hizo zitahitimishwa Novemba 3, 2012 katika viwanja hivyo na kuna uwezekanao Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chama hicho taifa akahudhuria.

DSCN5919Nassaro akizungumza huku mezani kukiwa na lundo la kadi za CCM za wananchi walioamua kuhama chama hicho na kujiunga na CHADEMA

Awanadi wagombea wa Chadema

DSCN5952Mh Nassari aliweza kuwatambulisha rasmi wagombea wa Chama chake (waliosimama) watakaoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 9 katika Halamashaur ya Mji Mdogo wa Usa River, uchaguzi unaotarajiwa kunfanyika Jumapili ya Novemba 4, 2012. Katika wagombea hao, mwanamke aliyejitokeza ni mmoja tu, Verian Mushi ambae anagombea mtaa wa Magadini.

Wagombea wa Chadema na Mitaa wanayogombania ni hawa wafuatao
1. Verian Mushi – Magadini,

2. Henry Benjamin Mpinga – Manayata

3. Ernest Makalla Shilla – Magadirisho

4. Exaud Jackson Mbise – Nganana

5. Richard Mohamed Ngungu – Kisambare

6. Malisa – Mji Mwema

7. Santrumini Filipo – Mlima Sioni (Lake tatu)

8. Frank Anael Msuya – Usa Madukani

9. William – Ngarasero

DSCN5908Baadhi ya viongozi wa Chadema Usa River na wagombea wao

Nassari azungumzia mafanikio ndani ya miezi 5 ya ubunge wake

Katika hotuba yake, Mh Nassari aliweza pia kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo amekwishayafanya kwa wananchi wake wa Arumeru tangu wamchague kuwa mbunge wao, takribani miezi mitano iliyopita.

Akiorodhesha mambo hayo harakaharaka, Nassari alisema kwamba amekwishakamilisha mradi wa maji ya kisima wenye thamani ya sh mil 60 kwa maeneo ya Ngobobo na Ngarenanyuki ambapo tayari wananchi wanayatumia

Akaeleza kuwa ameanzisha ligi ya mpira wa miguu kwa Kata zote za Jimbo lake na kudai kuwa vifaa vyote kwa ajili ya ligi hiyo vimemgharimu zaidi ya sh milioni 5. Ligi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 10 Novemba, 2012.

Alidai kuwa ameshiriki kwenye harambee nyingi za maji na kwamba ya karibuni amechagia kiasi cha sh milion 1.5, pia amechangia sh milioni 1 kwaya ya Jimboni kwake iliyomwaomba kuwasaidia.

Mambo mengine ni pamoja kusambaza vitabu vyenye thamani ya sh milion 38 kwa shule 15 za Kata, sehemu kubwa ikiwa ni msaada wa rafiki zake wa Marekani. Pia matengenezo ya choo kwa shule ya msingi Liganga, kuchangia vikundi vya kina mama.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO