Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KAMPUNI YA MAEGESHO YA MAGARI ARUSHA KAYIKA KASHFA NZITO

WAFANYAKAZI wa kampuni ya uwakala wa kukusanya ushuru wa maegesho ya magari jijini Arusha ya Kilimanjaro Printers(KPL) wameiingiza katika kashfa nzito kampuni hiyo baada ya kutuhumiwa kusababisha upotevu(kuiba) wa fedha za kigeni za watalii wa Kirusi kiasi cha dola 55,000.

Upotevu huo unadaiwa kutokana na wafanyakazi wa kampuni hiyo kubeba gari la kitalii lililokua na fedha hizo bila ya dereva wake kuwepo ndani ya gari alipokua ameliegesha.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya utalii ya Africa Smart Safari inayodai fedha hizo ambae ndiye mmiliki wa gari hilo lenye namba za usajili T302ABB Toyota Spacio,Sotet Mutambalike alisema gari yake ilichukuliwa kibabe na wafanyakazi wa KPL eneo la kituo cha mafuta cha Five Star kilichopo eneo la Unga ltd akijianda kupeleka fedha hizo benki.
Mutambalike alisema fedha hizo za kigeni ni malipo ya makundi manne ya watalii wa Kirusi waliokuwa wakitaka kutumia kampuni hiyo kwenda kupanda mlima Kilimanjaro.
Akieleza mkasa mzima kwa  waandishi wa habari alisema aliwahi kufuatwa na mfanyakazi wa KPL eneo la karibu na stand ndogo ya magari ya usafiri wa Jiji la Arusha{Vifodi} juu ya ushuru wa gari ya sh, 200/= na alitoa noti ya shilingi 10,000 lakini mfanyakazi huyo hakuwa na chechi ya kurudisha.
Alisema baada ya mfanyakazi huyo kukosa cheNchi ya shilingi 10,00 alimpa noti nyingine ya shilingi 5,000 ambayo nayo alikosa chenchi yake na ndipo alipomwambia kuwa anakwenda uwanja wa ndege kupeleka wageni na akirudi angempatia pesa yake.
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa juzi akiwa na gari ndogo iliyokamatwa alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Lewis ambaye baadae aligundua kuwa ni meneja wa KPL kuwa alikuwa akimtafuata na walikubaliana kukutana eneo gari lilikokamatwa.
‘’Meneja huyo alikuja eneo nilikokuwa nimegesha gari nikijiandaa kwenda kula ghafla aliniita chemba lakini cha kushangaza niliona wafanyakazi wake wakibeba gari yangu na niliwaambia kuwa humo ndani kuna fedha ngoja nitoe sikusikilizwa’’alisema
Alisema baada kuchukuliwa gari hilo  aliripoti katika ofisi ya mwanasheria wa Jiji la Arusha na ofisi hiyo iliuagiza uongozi wa kampuni ya KPL kutoa gari hilo kwani kosa ni la wafanyakazi wa kampuni yao ya  kukusanya ushuru kwa kutokuwa na chechi za kurudisha lakini walikaidi amri hiyo. 
Mutambalike alisema baada ya kuona hali hiyo aliripoti kituo cha kati cha polisi na kufungua faili lenye namba RB/13441/2012 juu upotevu wa fedha hizo na polisi ilikuwa ikiwasaka watuhumiwa wa kampuni ya KPL.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alikiri kuripotiwa kwa tukio hilo kituoni hapo na kudai kuwa linafanyiwa uchunguzi na ikibainika kuwa sheria na taratibu zilikiukwa wahusika wote watachukuliwa hatua.
“hilo tukio la upotevu wa dola lipo na tunalifanyia kazi na wahusika walijaribu kukiuka taratibu wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria’’alisema kamanda Sabas.
Naye Meneja huyo wa KPL Edward Lewis alipopigiwa simu alikiri gari hilo kushikiliwa na kampuni hiyo na kueleza kuwa mmiliki wa gari hilo hakutoa ushirikiano wowote.
Lewis alisema gari yao aina ya break Down yenye namba za usajili T61ADB ndio iliyovuta gari hilo na kupeleka ndani ya viwanja wa shirika la usagaji la Taifa{NMC}.
Meneja huyo alisema kuwa hawezi kujua kama ndani ya gari hilo kulikuwa na dola kwani yeye hakufanya kazi ya kulibeba gari hilo

Published by Pamela Mollel on October 25, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO