Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Prof. Alexander Nyangero Songorwa Mkurugenzi Mpya Wanyamapori

Prof. Alexander Nyangero Songorwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

TAARIFA KWA UMMA
VIONGOZI WAPYA WA IDARA YA IDARA YA WANYAMAPORI
WATEULIWA
Profesa Alexander Nyangero Songorwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori (Wildlife Division ) kuziba nafasi iliyokuwa wazi.
Kabla ya kuteuliwa Profesa Nyangoro alikuwa Profesa Mshiriki katika
Usimamizi wa Wanyamapori, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),
Morogoro. Pia ndiye aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo ya Usimamizi wa
Wanyamapori SUA.
Wakati huohuo, Profesa Jafari Ramadhani Kideghesho ameteuliwa
kuwa Mkurugenzi Msaidizi, kuiongoza Sehemu ya Matumizi Endelevu ya
Wanyamapori (Sustainable Utilisation of Wildlife Section). Kabla ya uteuzi
huo Profesa Ramadhani alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa
Wanyamapori katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.
Uteuzi huo umetekelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Bibi Maimuna Tarishi kwa mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa kifungu cha 6
(1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002. Utekelezaji wa
uteuzi huo ni kuanzia tarehe 24 Septemba 2012.
Mkurugenzi mpya wa wanyamapori, Profesa. Songorwa, ni msomi katika fani
ya Wanyamapori. Anayo shahada ya kwanza (B.Sc.) ya Sayansi katika Zoolojia
na Ekolojia ya Wanyamapori ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (mwaka 1987),
Shahada ya uzamili (MSc) katika Mipango na Maendeleo Vijijini ya Chuo
Kikuu cha Guelph, Ontario, Canada (1994) na shahada ya uzamivu (PhD) katika
Uhifadhi Maliasili ya Chuo Kikuu cha Lincoln, New Zealand (1999).
Kabla ya kujiunga na SUA mwaka 2001, Prof. Songorwa alikuwa mwajiriwa
wa Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzia mwaka
1982.
Akiwa Wizarani Profesa Songorwa alihudumu katka nafasi mbali mbali
zikiwemo Askari Wanyamapori, Mkuu wa Kanda na Msaidizi wa Mkuu wa
Mradi katika Pori la Akiba la Selous. Pia alihudumu kama Afisa Mwandamizi
katika Mradi wa Uhifadhi Shirikishi wa Wanyamapori, Makao Makuu, Dar es
salaam.
Naye Profesa Kideghesho siyo mgeni katika Idara ya Wanyamapori. Kabla ya
kujiunga na na SUA mwaka 1999 Prof. Kideghesho alikuwa mwalimu katika
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (CAWM-Mweka), Moshi
kuanzia 1993.
Kitaaluma Prof. Kideghesho ana shahada ya kwaza (B.Sc.) katika Kilimo ya
SUA (1993), Shahada ya Uzamili (MSc) katika Biolojia ya Uhifadhi ya Chuo
Kikuu cha Kent, Uingereza (1996), na Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Norway kilichopo mjini Trondheim
(2006).
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Simu 0784 468047
22 Oktoba 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO