Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TANZANIA YAUKWAA TENA UJUMBE BARAZA LA UTAWALA LA UMOJA WA POSTA DUNIANI

Tanzania imechaguliwa tena kuingia katika Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU), kipindi kingine cha miaka minne baada ya kuwa miongoni mwa nchi 40 kati ya nchi 192 wanachama wa umoja huo.

Katika uchaguzi wenye ushindani mkubwa na diplomasia ya hali ya juu, nchi nyingi zilikusudia kuingia kwenye Baraza hilo. Tanzania imekuwa moja ya nchi mbili za Afrika Mashariki, ikiwamo Uganda kushinda nafasi hizo. Nchi nyingi e za Africa zilizofanikiwa kuingia katika Baraza hilo ni Burkinafaso, Jamhuri ya Congo Brazaville, Ivory Coast, Misri, Gabon, Malawi, Morocco, Sudan na South Africa.

Mapema leo asubuhi, Balozi Hussein A. Bishar wa Kenya alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UPU akimshinda mwanamama Serrana Casco kutoka Uruguy. Nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mkuu iliyokuwa na ushindani mkubwa kati ya Mmarekani Denis Delehantty na Mswiss Pascal-Thienry Clivaz ambapo Clivaz alishinda nafasi hiyo.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame Mbarawa wakifurahia ushindi wa Tanzania kuchaguliwa katika Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani leo. Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi 40 zinazounda Baraza hilo, Kati ya nchi wanachama 192.

NA INNOCENT MUNGY DOHA, QATAR KWA HISANI YA BASHIR NKOROMO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO