Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Habari Mbaya: Milipuko ya mabomu yavuruga mbio za Boston Marathon; Watatu wafariki, mamia wajeruhiwa

Milipuko miwili ya mabomu iliyotokea karibu na mstari wa kumaliza mashindano ya mbio za Boston Marathon, nchini Marekani imewauwa watu wawili na zaidi ya 50 wengine walijeruhiwa Jumatatu.

Maafisa wa usalama walisema mlipuko wa tatu ulitokea kwenye maktaba ya John F.Kennedy iliopo katika mtaa mwingine wa Boston. Hakuna majeruhi yeyote aliyeripotiwa kutokana na mlipuko wa tatu na bado haijafahamika vyema kama mlipuko huo unahusiana na milipuko miwili iliyotokea awali kwenye mji huo.

Polisi wa Boston hawakusema kama milipuko ilikuwa sehemu ya shambulizi la ugaidi. Msemaji wa polisi alisema timu ya wataalamu wa kutegua mabomu walikuwa wakichunguza mifuko na vifurushi  vilivyoachwa kiholela kwenye tukio la milipuko ya awali lakini hakuna vifaa vingine vyovyote vinavyohusiana na milipuko vilivyopatikana.

Picha za televisheni zilionesha matukio ya kuogopesha, mtaa ulijaa  vifusi na damu, wafanyakazi wa huduma za dharura wakiwa wamebeba machela waliwasili mara moja kwenye mahala  uharibifu mkubwa ulipotokea.

Milipuko ilitokea mmoja baada ya mwingine ikipishana sekunde chache tu karibu na eneo la kumaliza mashindano ya mbio ambayo yaliwashirikisha wanamichezo wapatao 27,000. Mashindano yalisitishwa baada ya milipuko kutokea pamoja na usafiri wa njia ya metro katika eneo hilo.

Rais Barack Obama amelihutubia taifa na kutoa rambi rambi zake kwa waathiriwa akiahidi kwamba wahusika wa tukio hilo watapatikana, watafikishwa mbele ya sheria na watafahamu kwa nini wamefanya kitendo hicho kiovu.

Wakati huo huo polisi nchini Ungereza wanasema wanatathmini mipango ya usalama kwa ajili ya mbio za marathon zitakazofanyika Jumapili mjini London, baada ya milipuko ya mabomu kutokea huko Boston na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wawili.

Waandaaji wa marathon mjini London wanasema wamewasiliana na polisi kuzungumzia mipango ya usalama mara tu waliposikia tukio la milipuko la Boston nchini Marekani.

Maelfu ya wanariadha wamepangiwa kushindana katika mbio za London Marathon, zitakazofanyika chini ya muda wa wiki moja.

Taarifa na Voice of America

marathon

boston marathon explosions first responders

first responders boston marathon

first responders boston marathon

first responders boston marathon

Picha zote na mashirika ya habari ya Kimataifa kama AP

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO