Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MSIGWA: KIGOGO WA CCM ANAUZA PEMBE ZA NDOVU

CHADEMA 001Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa (mwenye sare nyeusi) na Mbunge wa Nyamagana, Mh Wenje wakielekeza uwanja wa Mwembtogwa mjini Iringa ambapo walikuwa na mkutano wa hadhara.  Picha na Said Ng’amilo.

elephant-tusksTembo akiwa katika hifadhi kwa uzima wake

tusksPembe za Ndovu.. Kila pembe mbili zinamaanisha tembo mmoja ameuwawa

temboTembo aliyeuwawa na kukatwa pembe.

***********************

UUZAJI wa pembe za ndovu anajulikana, sasa inakuwaje Serikali inashindwa kumkamata?” alisema Msigwa na kuahidi kulipua mabomu zaidi atakaporudi bungeni kwa maelezo kuwa anao ushahidi wa suala hilo.

Huo ulikuwa mkutano wa mwendelezo wa wabunge wa Chadema waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kuwapasha wananchi sababu ya kuchukuliwa hatua hiyo.
Wabunge hao walisimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje ya ukumbi, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.
Wabunge waliosimamishwa pamoja na Lissu ni Godbless Lema (Arusha Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Ezekiah Wenje (Mwanza Mjini) na Msigwa.

Hata hivyo, Lema na Lissu hawakuwapo katika mkutano huo wa jana ambao pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Mnyika kutoa hoja binafsi
Katika mkutano huo, Mnyika aligawa fomu kwa wananchi kuomba aungwe mkono wakati atakapotoa hoja binafsi bungeni juu ya mfumuko wa bei na umaskini nchini.
Mbunge huyo alisema wananchi wanakabiliwa na maisha magumu kutokana na hali mbaya ya uchumi.

“Napata uchungu ninavyoona Watanzania wakiishi maisha magumu kwa hiyo naandaa hoja binafsi ya kuwasilisha bungeni ili umma uelewe umuhimu wa suala hili,” alisema Mnyika na kuongeza kwamba atagawa fomu hizo kila atakapohutubia mikutano ya hadhara.
Dk Slaa na Usalama wa Taifa
Katika mkutano huo, Dk Slaa alidai kuwa maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wamegawanyika kutokana na makundi ya wanaotaka kuwania Urais mwaka 2015 kupitia CCM.

Dk Slaa alisema mgawanyiko huo ndiyo chanzo cha siri nyingi za idara hiyo kuvuja.

Aliwatuhumu baadhi ya wanachama wa CCM akidai kuwa wamekuwa wakiwavuta baadhi ya maofisa katika idara yao ili kuwasaidia kwenye harakati zao.

Chanzo: Gazeti Mwananchi, Picha na mitandao

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO