Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

POLISI WA INTERPOL KUTUMIKA KUWASAKA WATUHUMIWA WA KANDA ZA UCHOCHEZI WA KIDINI WALIOTOROKA MWANZA

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu

POLISI wa Kimataifa (Interpol Police) kutumika kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa wawili wa Kanda za uchochezi wa Kidini waliotorokea katika Mataifa ya India na Amerika wanaosakwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza .

Tamko hilo limetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu ametoa tamko hilo hii leo ofisini kwake.

Amesema kwamba tayari jeshi hilo limetoa taarifa kwa Askari wa Interpol na Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es salaam  ili kusaidia kuwakamata na kuwarejesha watuhumiwa wawili ambao ni viongozi wa Kidini wanatuhumiwa kwa kutoa Kanda (DVD na CD) zilizo na maudhui ya uchochezi wa kiimani kwa madhehebu ya Kidini nchini. (ZAIDI OFYA PLAY MSIKILIZE)

“Tangu mwezi wa Februari mwaka huu tulitoa rai ya kuwatafuta watu watatu ambao ni viongozi wa kidini kwa tuhuma hizi za uchochezi lakini hadi sasa tumefanikiwa kumkamata mmoja wao aitwaye Imamu Hamza Omary na kumfungulia mashitaka huku yukiwa tayari tumeisha mfikisha katika mahakama ya Wilaya kuendelea na kesi”alisema Kamanda.

Kamanda Mangu amewataja watuhumiwa wengine wanaotafutwa na jeshi hilo na wanaodaiwa kutoroka nchini kwa ni Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kiongozi wa Taasisi ya kidini ya Thaqeeb iliyopo Kata ya Nyamanoro Wilayani Ilemela na Askofu Augustine Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field Evangelist na Mkurugenzi anayemiliki kituo cha Redio Kwa Neema FM cha Jijini Mwanza ambacho kimefungiwa na TCRA miezi sita kwa ukiukwaji wa maadili.

“Hawa wawili tumeamua kuwashirikisha polisi wa Interpol ili kuwakamata na kuwarejesha nchini ili kuwaunganisha na kesi tuliyomfungulia mwenzao Imamu Omary na tunasikia kuwepo kwa taarifa kuwa Sheikh Ilunga kuwa yupo nchini India na Askofu Mpemba yupo nchini Marekani wanakodaiwa kutorokea,bado tutahakikisha tunawakamata tu ni vyema wakajisalimisha kabla ya hawajakamatwa ”alisisitiza.

Kamanda Mangu ametoa muda wa siku nne kwa wafanyabiashara  wanaouza na kusambaza Kanda (DVD na CD) za uchochezi ziliotolewa na watuhumiwa hao  wanaotafutwa na jeshi hilo na zingine zenye maudhui ya uchochezi wa kiimani wa kidini kuzisalimisha kwa ihali yao kwenye vituo vya polisi  kabla ya kuanza opresheni ya kuzisaka Jijini Mwanza na Wilaya zote za Mkoa huo na hata ile ya jirani.

Kanda zilizopigwa marufuku ni pamoja na Unafiki katika Sensa, Bakwata tawi la Kanisa,Mauaji ya Sheikh Abdu Rogo wa Mombasa na Mwisilamu rudisha Imani zilitolewa na Sheikh Ilunga, Ndege wote walie akilia Bundi Uchuro ya Imamu Omary na Inuka chinja ule iliyotolewa na kusambazwa na Askofu Mpemba.

Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri kwa jeshi hilo ili kuweza kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na watu wanaoendelea kusambaza na kuziuza kanda hizo kwa usiri ili kuwafikisha katika chombo cha sheria kutokana na kueneza uchochezi wa kiimani ka madhehebu ya kidini jambo ambalo linahatarisha amani ya nchi na huweza kusababisha machafuko zaidi ya kidini.

TAARIFA HII NI KWA HISANI YA G SENGO BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO