Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU TUKIO LA AJALI YA MAPOROMOKO YA ‘MORAM’ ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA TATU JIJINI ARUSHA

TUKIO LA AJALI YA MAPOROMOKO YA MORAMU ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA TATU

Mnamo tarehe 01/04/2013 muda wa saa 4:40 asubuhi huko Moshono Tanganyika Parkers kwenye machimbo ya moramu, watu kumi na tano (15) wakiwa katika uchimbaji na upakiaji wa moramu waliangukiwa na kifusi cha udongo wa moramu na  hatimaye kusababisha vifo vya watu kumi na tatu (13) na wawili kujeruhiwa.

Taarifa hizo zinaeleza kwamba, muda wa saa 4:00 asubuhi watu hao walikuwa wanapakia moramu katika magari mawili ambayo ni Scania lenye namba za usajili T. 886 BDA na jingine ni aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T. 109 AYB.

Ilipofika muda huo wa asubuhi, kifusi cha moramu kiliporomoka ghafla na kuwafunika watu wote waliokuwa katika eneo hilo.  Mpaka hivi sasa Jeshi la Polisi Mkoani hapa limetambua miili ya marehemu pamoja na majeruhi. Waliofariki katika ajali hiyo ni:- Julius s/o Peter Palangyo (56) mkazi wa Nkoaranga Wilayani Arumeru, Fredy s/o Loserian (21) mkazi wa Tanganyika Parkers Moshono,Christopher s/o Laurent (24) kondakta na ni mkazi wa Kijenge, Gerald s/o Jacob maarufu kwa jina la kababu (24) mkazi wa Moivaro, Gerald s/o Masai (33) mkazi wa Tanganyika Parkers, Japhet s/o Amani Kivuyo (27) mkazi wa Moshono na Mwenda s/o Stephano (25) mkazi wa Moivaro.

Wengine ni Elias s/o Fanuel (28) mkazi wa Tanganyika Parkers, Barick s/o Kipara (26) mkazi wa Moshono, Seurii s/o Raphael maarufu kwa jina la mbu (24) mkazi wa Moshono, Alex s/o Marick (23) dereva na ni mkazi wa Moshono, Hassan s/o Mussa (24) mkazi wa Moshono na wa mwisho ni Gerald s/o Nerujangi (45) mkazi wa Moshono.

Majeruhi katika ajali hiyo ni Samwel s/o Gunda (29) kondakta, mkazi wa Moshono na Mariaki s/o Lenanu (48) mkazi wa Tanganyika Parkers ambao wote walikuwa wamelazwa katika hospitali ya Mount Meru hiyo jana na Samwel s/o Gunda amesharuhusiwa huku mwenzake akiendelea kupatiwa matibabu. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mount Meru. Asanteni kwa kunisikiliza.

Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,

Kamishna Msaidizi wa Polisi,

(ACP) Ibrahim Kilongo

Tarehe 02/04/2013

**********************************************************************************************************************

WAKATI HUO HUO…

IMG_0643Serikali imesimisha kwa muda machimbo ya morom yaliyoko katika Kata ya Moshono Jijini Arusha baada ya kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi 2 ili kuweza kufanya tahmini ya kimazingira mazingira ya machimbo hayo kwa kuwa ni muhimu kwa shughuli za ujenzi wa mkoa hapa.

Uamuzi huo wa Serikali umeelezwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akihudhuria ibada maaalum ya ya pamoja kuaga miili ya marehem waliokufa katika machimbo hayo kwa kufukiwa na kifusi, zoezi lililofuatiwa na kuzuru eneo la ajali na kujionea hali halisi. 

Mh Pinda pia aliwatembelea majeruhi waliolazwa hospitali ya Mt Meru na pia kuwapa pole wafiwa.

Akiwa katika eneo la ajali, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi kuwa hawajafunga machimbo hayo moja kwa moja bali yamesitishwa kwa muda kwa ili kuboresha mazingira ya machimbo hayo katika kuepusha hatari nyingine, kutokana na umuhimu wake katika ujenzi pamoja na kipato kwa wananchi..

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO