Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Rais Wa Zanzibar Dr Ali Shein,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr Gharib Bilal,Makamu wa Kwanza Wa Rais Zanzibar Maalim Self Sharrif Hamad,Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd Washiriki Dua Maalum Ya Kumswalia Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude',Mchana Huu Zanzibar.

Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib 'Diamond Plutnum' (kulia), akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao  Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja. TAARIFA HII NA PICHA NI KWA HISANI YA HAKINGOWI.COM

PICHA ZIFUATAZO ZINAONESHA NAMNA WANANCHI WA KAWAIDA, WADAU WA SANAA  NA WASANII MBALIMBALI WAKISHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAZIKO YA BI KIDUDE. PICHA KUTOKA AUDIFACE JACKSON BLOG


Jeneza la bibi likielekea msikiti kwa ajili ya kusaliwa


Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi R.I.P..........KIDUDE BINTI BARAKA


Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwamarehemu bi Kidude, Zanzibar

Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi)

Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude

Guru G na Mh Bhaa mazikoni

Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude

Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO