Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA TV: USHAHIDI WA MH. PETER MSIGWA KUHUSU UJANGILI UNAOANGAMIZA TAIFA

Msigwa px



Huu ndiyo ushahidi wa video uliowasilishwa ndani ya bunge na Mheshimiwa Peter Msigwa (MB), Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, unaonesha namna ambavyo Sekta ya Wanyamapori iko hatarini kutokana na uwindaji haramu unaofanyika ndani ya mbuga, mapori na hifadhi zetu Watanzania.

Video hiyo, aliyoiita ya ushahidi alioutoa bungeni kwa Spika Anne Makinda wakati akiwasilisha bajeti mbadala ya wizara hiyo mwezi Mei, inaonyesha wawindaji wa kampuni ya Green Mile Safaris Ltd wakifanya uwindaji kinyume na taratibu na sharia.

Video hiyo ya inayoitwa Tanzania Hunting Trip Season 2012’, iliyotengenezwa mwaka 2012 na Green Mile Safaris kwa lengo la matangazo, inaonyesha wawindaji wenye asili ya Kiarabu wakifanya ‘ufundi’ wa kuua wanyama wakiwa ndani ya gari pia wakitumia baadhi ya bunduki kali kama Sub Mashine Gun (SMG) zenye viwambo vya kuzuia sauti.

Pia mmoja wa wawindaji katika moja ya sehemu za video hiyo, anaonekana akimfundisha kuwinda wanyama wadogo na ndege mvulana mwenye umri wa kati ya miaka 12-15.

Aliwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa ameamua kutoa ushahidi huo kutokana na Serikali kutochukua hatua zozote kuhusu kampuni za uwindaji zinazokiuka sheria.

Msigwa alisema wawindaji hao wanaonekana wazi kukiuka sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009 kwa kuwinda wanyama wadogo na kutumia magari binafsi kuwakimbiza wanyama na kuwaua.

Waziri huyo kivuli ambaye pia ni mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), alisema kampuni hiyo ilifanya makosa 11 lakini Serikali iliiacha iendelee kuwinda bila kuchukua hatua yoyote.

“Kutokana na ubutu wa Serikali hii katika kusimamia rasilimali zetu, kuzuia uwindaji holela unaokuza ujangili na kutishia hatima ya maliasili na utalii nchini, kampuni hii imekiuka kifungu namba 42 cha Sheria ya Wanyamapori ya  2009, kinachoeleza kuwa mtu yeyote atakayemjeruhi mnyama atatakiwa kutumia juhudi zote kadiri ya uwezo wake kumuua mnyama ndani ya muda mfupi iwezekanavyo,” alisema Msigwa.
Msigwa aliitaka Serikali kuzifanyia uchunguzi wa kina kampuni zote za uwindaji nchini ikiwa ni pamoja na Green Mile.

“Waziri wa Maliasili na Utalii awawajibishe watendaji wa wizara ambao wameshindwa kutimiza na kutekeleza wajibu na majukumu yao.

Akijibu tuhuma hizo jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikiri kuwapo kwa video hiyo na kuwa ameshaipa kazi Idara ya Wanyamapori kufanya uchunguzi juu ya mambo yaliyomo na iwapo watabaini uhalisia, watatoa majibu stahiki.

“Ni kweli video hiyo ndiyo iliyowasilishwa rasmi bungeni na mimi nilichukua hatua za haraka ikiwamo kuitask (kuipa kazi) Idara ya Wanyamapori kuangalia authenticity (uhalisia) wa video hiyo.

STORI: MWANACHI NEWSPAPER

VIDEO: CHADEMA TV

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO