Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKUTANO WA 29 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (MEAC) KUFANYIKA SEPTEMBA 20-2014 JIJINI ARUSHA

MKUTANO wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kuanza Septemba 20, 2014 katika jiji la Arusha.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji na Biashara wa wizara hiyo Dk. Abdullah Makame alisema katika mkutano huo baraza linatarajia kujadili agenda mbalimbali na kutolea maamuzi masuala kadhaa.

Alisema katika mkutano huo watazungumzia na kuadhimisha aina mpya ya hati ya kusafiria ya kielectroniki zikiwemo sampuli za hati ya kusafiriaza kibalozi za maofisa na wananchi wa kawaida.

'Hati  hizo za kusafiria zitasaidia  kukuza biashara na soko la kimataifa na kusafiria nchi mbalimbali  kwani za awali zilikuwa  haziruhusiwi'' alisema Dk. Makame.

Aliongeza kuwa katika baraza hilo pia kuatajadiliwa mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa dira ya maendeleo ya Afrika Mashariki 2050.

'' Moja ya ajenda itakuwa ni kuandaa mapendekezo ya mpango mwelekeo wa shughuli mbalimbali kama vile  kuaandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki na sarafu moja ya nchi zilizopo katika jumuia hiyo,' alisema.

Akizungumzia ni vipi Tanzania imekuwa ya kwanza kukubali kuwa na sarafu kuliko nchi nyingine alisema ''Tanzania imekubali kwa haraka kwa sababu ilikuwa kinara katika kujadili umoja wa forodha na umoja wa fedha,''.


Alisema Baraza la Mawaziri huwa linaundwa na Mawaziri wa Ushirikiano wa Afrika Masahariki pamoja na mawaziri wengine kutoka nchi wanachama na baraza hilo huwa linakutana mara mbili kwa mwaka.

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji  na Biashara wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MEAC), Dk. Abdallah Makame (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuia ambao utafanyika Septemba 20, 2014 jijini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Wizara hiyo, Anthony Ishengoma.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji  na Biashara wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MEAC), Dk. Abdallah Makame (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano huo.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uzalishaji  na Biashara wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MEAC), Dk. Abdallah Makame (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano huo.

. Kulia ni Ofisa Habari Idara Habari Maelezo, Frank Mvungi na  Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Anthony Ishengoma.

Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Maofisa wa Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Teodos Komba na Mtaalamu wa Mawasiliano, Faraja Mgwabati.

Mkutano ukiendelea

CREDIT: WOINDE SHIZZA-LIBENEKE LA KASKAZINI

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO