Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA AFRIKA NA CHINA JIJINI ARUSHA TANZANIA, RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA

Mgeni Rasmi wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, Rais wa Zimbabwe,Robert  Mugabe akihutubi usiku huu kweye kongamano hilo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,ambapo Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China linafanyika na mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (aliyeshikwa  mabepa) akiwasili usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kufungua kufungua  Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China.

RAIS Jakaya Kikwete  akipewa tunzo  ya Heshima ya juu ya Kuhamasisha Amani na Utulivu katika Bara la Afrika na Rais wa Umoja wa Vijana Afrika (PAYU),Francine Furaha Muyumba .Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Vijana  wa  Umoja wa Afrika,pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh.Mboni Mhita

  Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu zake kwa washiriki wa   Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.

  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe,kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana

Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipowasili jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kutoa salamu kwa washiriki wa   Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe. Pichani kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh.Stephen Masele.

 

Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akizungumza jambo na Rais wa Zimbambwe,Mh.Robert Mugabe mara mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchaa.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo  na Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha..

PICHA NA IKULU

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO