Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lowassa akutanisha Balozi wa Japan nchini na Viongozi wa Monduli kujadili Maendeleo yao

Pichani Mhe Edward Lowassa alipokutana na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida katika kikao cha pamoja na Mbunge wa Monduli Julius Kalanga, wakiongozana na Mkuu wa Wilaya Francis Mitti, DED Ephraim Ole Nguyainey, M/kiti wa Halmashauri Isaack Joseph.

Wengine katika kikao hicho ni Mhandisi wa Wilaya Daudi Sebyiga, na Mganga mkuu wa wilaya Zavery Venela na kikao kimefanyika ofisini kwa Lowassa Jijini Dar es salaam kwa lengo la  kuishukuru Serikali ya Japan kwa misaada ambayo wamekuwa wakiipatia wilaya ya Monduli na pia kujadili mipango mipya ya maendeleo ya Wilaya hiyo.
Mh Lowassa na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Monduli wakiwa katika kikao na Balozi wa Japani nchini
Mh Lowassa akiwa na Balozi wa Japan nchini Bw Yoshida


Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO