Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nape Ajikanyaga DW Kuhusu Kufungia Mawio na Kuzuia Matangazo ya Bunge live

Akihojiwa na DW amesema ni kweli sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ni mbovu na inapelekwa bungeni kuibadilisha. Alipoulizwa kwamba kama amekiri sheria hiyo ni mbovu ikiwa itafutwa na maamzi ya kulifungia Mawio yatabatilishwa kwa vile yalifanyika kwa kutumia sheria mbovu? Akasema sheria hata kama ni mbovu lazima iheshimike hivyo maamzi yatabaki pale pale.

Kuhusu bunge kurushwa live Nape amesema watumishi wa serikali walikuwa wakiiba muda wa kazi kutazama bunge. Alipoulizwa kwa nini hatua za kiutendaji zisichukuliwe badala ya kusitisha matangazo na kwa nini mwanzoni alisingizia gharama. Akajibu kwamba suala hilo si la serikali bali bunge "Kwanza hili suala si la serikali, bunge liliona ni kuna redio 125 nchi hii na wote hawawezi kuleta mitambo yao hapa hivyo wakatengeneza studio ambayo redio zote zinaweza kupata matangazo" alisema.
 

Alipobanwa kwamba kwa nini redio na Tv zilizo na uwezo wa kurusha moja kwa moja zilizuiliwa? Akajibu, mbona South Africa wanafanya hivyo na hakuna malalamiko? "Nchi nyingine kama South Africa inaonyesha masaa 8 live na baada ya hapo wanarekodi huko mbona hawalalamiki
CHANZO: THE CHUMA BLOG
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO