Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JUMUIYA YA WAISLAMU WILAYA YA HAI YATAMBUA MCHANGO WA FREEMAN AIKAEL MBOWE KATIKA KUDUMISHA UMOJA WA KITAIFA





Ni jambo la kawaida duniani kote kutambua mchango au juhudi za mtu au kiongozi katika kusimamia, kufanikisha au kuwezesha jambo fulani kutokea kwa namna yoyote ile.

Hiki ndicho kilichotokea wilayani Hai, ambapo jumuiya ya WAISLAMU Hai imemtunuku cheti cha amani (PEACE AWARD) Mbunge wa Hai ambaye pia ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nchini na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa.

Cheti hicho kikiwa ni ishara ya kuonesha thamani ya mchango wa Mh. Mbowe kupitia nafasi zake za kisiasa na uwakilishi, hasa katika kudumisha umoja, upendo,  haki, amani, mshikamano, ushindani wa hoja nk. kwa wananchi wa Hai na Tanzania kwa ujumla.

Hata hivyo pamoja na mchango mkubwa huo wa Mh. Mbowe katika kujenga umoja wa kitaifa kutambuliwa na Jumuiya ya WAISLAMU, vilevile cheti hicho ni salamu za kumpa moyo Mh. Freeman Mbowe katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa wananchi wa Hai na taifa kwa ujumla, licha ya changamoto mbalimbali anazokutana nazo kisiasa, kijamii na kiuchumi. 


Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO