Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MBUNGE WA VITI MAALUMU CATHERINE MAGIGE AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA NA WALE WAONAOISHI KATIKA MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA


 Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Catherine Magige akimkabidhi mkurugenzi na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Faraja  orphance kilichopo jijini hapa,kituo hichi cha watoto yatima kina jumla ya watoto 200 na kati ya watoto hao watoto 30 wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

wa pili kushoto  mbunge wa  viti maalumu akiwa anateta jambo na katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan ,wakwanza kulia ni katibu wa kanda ya kaskazini msikiti wa  Twariqatul  ndugu Abdi Ramathani


 mbunge wa viti maalumu akiwa anamkabidhi zawadi za iddi mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Samaritan villege Jospephat Mmnyi

 mbunge wa viti maalum akiwa pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima na wasiojiweza cha Faraja ,mkurugenzi wa kituo hicho pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha
 mbunge wa viti maalumu akiwa amembeba moja ya mtoto aliotelekezwa na mama yake akiwa mdogo anaeishi katika kituo cha watoto yatima cha Faraja kilichopo jijini hapa wakati alipowapelekea zawadi ya iddi

 mbunge wa viti maalumu akimkabidhi msaada wa chakula mmoja wa kijana wa kito cha Zawiani wakati alipotembelea kutoa zawadi za  sikukuu ya iddi
 mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anapewa maelezo mafupi katika maabusu ya watoto Arusha ,Ambapo aliaambiwa mahabusu hiyo inauwezo wa kubeba watoto 50 wakike wakiwa 10 na wakiume wakiwa 40  lakini kwa sasa ina jumla ya mahabusu 12 tu na wote wakiwa ni wanaume (picha na Woinde Shizza,Arusha )
 Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anamkabidhi mbuzi ,mchele na mafuta kiongozi wa kituo cha mahabusu Arusha Mussa Mapunda ikiwa ni zawadi ya idi kwa watoto hao
 vijana wa kituo cha Zawiani wakisala kabla ya msaada kutolewa wakiwa na mbunge wa viti maalumu pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi

 Habari picha na  Woinde shizza,Arusha
 Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Catherine Magige leo amekabidhi  msaada wa mbuzi watano ,chakula  na mafuta kwa vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja watoto wanoishi katika mahabusu ya watoto mkoani hapa ili kusherekea sikukuu ya idi .

Akikabidhi msaada huo kwa katika vituo hivyo alisema kuwa watoto hao wanapaswa kusherehekea sikukuuu  ya iddi  kama wengine wanaoishi na wazazi wao majumbani kwao .

Alisema kuwa vitu vyote hivyo alivyovigawa katika vituo vyote alivyo vitoa ametoa kwa moyo wake  wote ,ambapo alisema kuwa yeye kama mama ameguswa na akaamua kwenda kuwapa watoto hawa msaada huo ili nao wakisherekea sikukuu hii wajisikie nao wapo na wazazi wao. 

"napenda kuwasihi wananchi wajijengee tabia ya kusaidia watoto hawa yatima pia wajifunze kutembelea hata hawa watoto mahabusu ata kama awana watoto katika mahabusu hizi lakini wanaweza wakatoka na misaada na kuamua kupelekea watoto hawa yatima au hawa watoto walioko mahabusu kwani ni watoto na wanahaki ya kupendwa kama watoto wengine"alisema Magige

Alivitaja vituo ambavyo vimepewa msaada kuwa ni pamoja na Faraja ophas,Samaritan villege,kituo cha watoto yatima  na wasio jiweza cha Zawiani pamoja na Mahabusu ya watoto  Arusha

 Wakati huohuo, Ofisa Msimamizi wa kito hicho , Mussa Mapua  aliiomba Serikali kujenga uzio katika mahabusu hiyo ili kuzuia watu wenye nia mbaya kuingiza dawa za kulevya au wale watoto ambao ni wakorofi kutoroka.

Aidha  alisema kuwa pia  wanahitaji wanasheria wa watoto hao ili kesi zao zilizoko mahakamani ziishe kwa muda mfupi, tofauti na hali ilivyo sasa huku akisema kuwa mahabusu hiyo kwa sasa inawatoto wa kiume 12 wote wakiwa ni wanaume

"unajua  kesi zinachelewa kutokana na kukosekana kwa wanasherisa wa kuwatetea watoto  hivyo tunaomba serikali ijitaidi kutuletea mwanasheria wa kutetea watoto hawapia napenda kutumia nafasi hii kuliomba  Jeshi la Polisi kuwa makini katika upelelezi wa kesi mbalimbali ikiwamo kuzingatia umri wa watoto ili kuepuka kuwapeleka wakubwa katika mahabusi hiyo "alisema Mapua



Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO