Msemaji wa Pamba, Gervas Mbaya (kushoto), akiteta na Slyvester Joseph-VesterJtz @BMG (kulia).
Na BMG
Baada ya jana timu ya soka ya Pamba ya Jijini Mwanza, kupata nafasi ya kucheza ligi daraja la
kwanza kutokana na timu ya Abajalo Fc ya Jijini Dar es salaam kupoteza pointi
sita kwa kosa la kumchezesha mchezaji wa Kagera Sugar katika michuano ya ligi
daraja la pili, timu hiyo imeeleza furaha yake sambamba na mikakati iliyopo katika
kuelekea michuano ya ligi daraja la kwanza.
Akibonga na
VesterJtz wa BMG, Msemaji wa timu ya Pamba, Gervas Mbaya, amesema wamepokea
maamuzi yaliyotolewa na TFF kwa shangwe kubwa baada ya kushinda rufaa waliyokuwa
wameikata wakilalamikia ushindi wa timu ya Abajalo Fc.
Amesema
ndani ya siku mbili zijazo, uongozi wa timu hiyo utakutana ili kupanga mikakati
ni lini timu ya Pamba ianze kufanya mchakato wa usajili ili timu iingie kambini
kwa ajili ya maandalizi ya mapema kuelekea michuano ya ligi daraja la kwanza.
Msemaji wa Pamba, Gervas Mbaya (kushoto), akiteta na Slyvester Joseph-VesterJtz @BMG (kulia).
Itakumbukwa kwamba timu ya Pamba SC ya Mwanza na The Mighty
Elephant ya Songea zilikata rufaa TFF kuilalamikia timu ya Abajalo FC kwa
kumtumia mchezaji wa Kaliua City ya Tabora, Laurence Mugia, wa Kagera Sugar katika
michezo ya mtoano wa Ligi daraja la pili kwa ajili ya kupanda daraja la kwanza
ambapo baada ya kushinda rufaa hiyo timu zote zilijinyakulia pointi tatu na
magoli matatu huku Abajalo ikipoteza pointi sita na hivyo kupoteza nafasi ya
kucheza ligi daraja la kwanza.
Bonyeza HAPA Kusikiliza Zaidi. Au Bonyeza Play Hapa Chini.
0 maoni:
Post a Comment