Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Vifaa vya kijeshi vilivyooneshwa katika sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutimiza Miaka 50

Watoto wa Halaiki wakionesha umbo la picha za Rais wa Kikwete na Rais Shein na maneno yanayosomeka Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

 

Hiki ni kifaru

Kifaru cha kivita kikipita mbele ya wanahabari na wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo

Makombora mazito ya kivita yakipita

Askari wa miamvuli ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wakishuka kwenye uwanja wa Uhuru baada ya kuruka kwenye ndege umbali wa mita zaidi ya elfu 4000 angani.

Wakienda kutoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete akiwapongeza askari hao wa miamvuli mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Uhuru

Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu

 

Askari kwa kikosi cha komandoo wakiingia uwanjani kwa ajiri ya heshima kwa amiri jeshi mkuu huku wakiwa wameshikilia bunduki za AK47

Komandoo kutoka kikosi cha Sangasanga wakiingia kwa mbwembe kumuonyesha Amiri Jeshi Mkuu jinsi wanavyojilinda wakati wakiwa wamevamiwa, kikosi ambacho kimeonesha buruduni ya hali ya juu

Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.

moja ya kusherehea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Kikosi cha Makomando wakionesha mbele ya Mhe. Rais, wageni waalikwa na wananchi mafunzo waliyopitia

 

Watoto kutoka Tanzania Bara na Zanziba wakionesha utaalamu wa kucheza ngoma

Kikundi cha Wasanii mbalimbali wakiimba wimbo maalum wa pamoja kuhusu miaka 50 ya Muungano.

Ndege za kivita nazo zikipita angani .

 

Mwanajeshi akitua na mwanvuli kutoka angani mita 4000 kutoka usawa wa bahari

Picha: Vyazo Tofauzi, zaidi  Reginald Philip na Ofisi ya Makamu wa Rais

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO