Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

PINDA AANDAA CHAKULA KWA TIMU YA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU ILIYOTWAA KOMBE LA DUNIA; WAALIKWA BUNGENI

PG4A6024Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa nahodha msadidizi wa timu ya soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, Frank William, kombe la ubingwa wa dunia wa soka la watoto wa Mitaani wakati alipowaandalia chakula cha mchana kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo.

Keptain  Msaidizi wa  Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) Frank William akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo .

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia wakiwa wameshikilia Kombe la ushindi la Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC)baada ya timu hiyo kutembelea Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo.

Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ambao ni Bingwa wa Dunia kwa mpira wa miguu kwa watoto wa mitaani wakiwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu leo mjini Dodoma mara baada kutembelea Bunge Maalum la Katiba .

PG4A6063Wachezaji wa Timu ya Soka ya  Tanzania  ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa wa Dunia  wakipata Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11, 2014. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)

PG4A6085Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na  wachezaji wa Timu ya Soka ya  Tanzania  ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa wa Dunia  katika Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11, 2014.

Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu, Stori Na Magreth Kinabo –Dodoma

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO