Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

DC wa Hai Aamuru Mwalimu Akamatwe Baada ya Kushindwa Kutaja Jina Lake



Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa (pichani) anadaiwa kumweka mahabusu mwalimu mmoja kwa kushindwa kutaja jina la kiongozi huyo.Tukio hilo lilianza kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii jana ikielezwa kuwa mkuu huyo wa wilaya alimtaka mwalimu huyo achague kupiga ‘pushup’ 20 au polisi wakamkamate na kumsweka mahabusu.Kutokana na tukio hilo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimemjia juu mkuu huyo wa wilaya kikidai kuwa maswali aliyokuwa akiyauliza mteule huyo wa Rais John Magufuli hayakustahili na wala hayakuwa ya kitaaluma.CWT ilisema katika ziara hiyo ambayo mkuu wa wilaya alitembelea shule mbili, aliwataka walimu wataje jina lake (la DC), shule imeshika nafasi ya ngapi kitaifa na wataje majina ya magazeti ya Serikali.Pia, inadaiwa katika maswali yake hayo, mkuu huyo wa wilaya alimtaka mwalimu huyo ataje tofauti ya CUF (chama cha siasa) na CAF ambalo ni Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika.Mkuu huyo wa wilaya alipopigiwa simu jana asubuhi ili azungumzie tuhuma hizo, alisema yuko kwenye kikao na kuomba apigiwe simu baadaye.Alipopigiwa simu mara ya pili mchana alijibu: “Siwezi kuzungumzia suala hilo, nipo kwenye kikao na walimu tangu asubuhi waandishi wananipigia simu nawaambia hawanielewi.”Hata hivyo, jioni alipopigiwa tena kwa mara ya tatu na kuulizwa tena sababu za kumuweka mahabusu mwalimu huyo alijibu: “Sikumuweka ndani mwalimu huyo kwa sababu ya kushindwa kutaja jina langu, isipokuwa ni kwa sababu ya kunikosea nidhamu.”Jana, mwalimu huyo wa Shule ya Sekondari Lerai, Erasto Mhagama alisema aliwekwa mahabusu wiki iliyopita kuanzia saa 8:30 mchana hadi saa 2:00 usiku alipoachiwa huru.Kwa mujibu wa mwalimu huyo, polisi walimweleza kuwa amewekwa mahabusu kwa amri ya mkuu wa wilaya bila kupewa sababu za kutendewa hivyo.Mwalimu huyo alisema kabla ya kukamatwa kwake, DC Byakanwa alifanya kikao na walimu na alianza kwa kuwauliza wangapi wanamfahamu kwa majina yake, lakini wote walikaa kimya.Baada ya kimya hicho, mkuu huyo wa wilaya aliwapa karatasi walimu wote ili waandike majina yake, lakini wote walishindwa kuliandika.Alisema baada ya muda, mkuu huyo wa wilaya aliwataka waandike nafasi iliyoshika shule hiyo kwenye Mtihani wa Taifa kwa mwaka 2015, mwalimu mmoja inadaiwa alishindwa kuandika.Mwalimu huyo alifafanua kuwa mkuu huyo wa wilaya alimfuata yeye na kumtaka aeleze Halmashauri ya Wilaya ya Hai ina shule ngapi, alimjibu kuwa asingeweza kutaja kwa kuwa hakuwa na takwimu sahihi.Alisema majibu hayo yalimfanya kiongozi huyo apige simu polisi na kuwaagiza wafike shuleni hapo haraka, lakini kabla hawajafika, alimwita pembeni na kumtaka achague adhabu moja kati ya kwenda mahabusu au kupiga ‘push-up’.“Aliniambia nichague kupiga push-up 20 au niende mahabusu nilimwambia siwezi kupiga push-up kwa sababu nina matatizo ya kiafya. Nikachukuliwa nikapelekwa polisi Bomang’ombe,”alisimulia mwalimu huyo.Mwenyekiti wa CWT mkoani Kilimanjaro, Omary Mchome alisema kitendo kilichofanywa na mkuu huyo wa wilaya hakikubaliki na ni kinyume cha maadili ya kitaaluma na ya utumishi wa umma.“Hiki ni kitendo cha udhalilishaji, CWT hatutavumilia tutatoa tamko kali. Kumweka mtu ndani kwa sababu ameshindwa kujibu maswali ni kudhalilisha taaluma ya ualimu,” alisema Mchome.Mwenyekiti huyo alisema baada ya kupata taarifa hizo, viongozi walikwenda kwenye shule mbili ambazo mkuu huyo wa wilaya alizitembelea wakapatiwa taarifa ya kadhia hiyo.“Baada ya kupata taarifa nilimtuma Katibu wa CWT Mkoa wa Kilimanjaro na wa Wilaya ya Hai kufanya mahojiano na walimu waliokuwapo katika kikao hicho, walisema waliulizwa maswali ambayo si ya kitaaluma.“Eti unamuuliza mwalimu taja jina langu, shule yako imeshika nafasi ya ngapi kitaifa, taja magazeti ya Serikali. Haya mambo yanaingiaje katika taaluma? Na kama mtu huyafahamu ni kosa?” alihoji Mchome.Mwenyekiti huyo alisema katu hawatafumbia macho suala hilo kwakuwa ushahidi wanao na jana au leo walitarajia kupeleka barua rasmi ya malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Source: Gazeti Mwananchi
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO