Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RC Gambo Atoa Siku 7 kwa Halmashauri ya Longido Kujieleza Kuhusu Kupata Hati ya Mashaka

Halmashauri ya Wilaya ya Longido imepewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) kwa mwaka fedha kuanzia 2015 hadi 2017.

Akitoa agizo hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amesema halmashauri kupata hati ya mashaka kwa hoja zinazojibika na zinazojirudia kila mwaka ni uzembe wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.
“Watumishi bado wapo wachache wanaofanya kazi  kwa mazoea bila ya kufuata sheria na taratibu za kiutumishi”.

Ameuwagiza uongozi wa halmashauri ya Longido kutoa barua za onyo kwa watumishi wote waliotajwa kwenye taarifa ya mkaguzi wa nje ili iwe fundisho kwa watumishi wote umma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,amesema ifike wakati sasa viongozi kutoonea huruma mtumishi yoyote anaebainika ana makosa, kwani hoja nyingi katika halmashuri hiyo zimekuwa zikijirudiarudia kila mwaka.
Amesema  hatua madhubuti ni lazima sasa zichukuliwe ili kudhibiti tabia hii ya mazoea ya hoja kujirudiarudia kila mala.

Akisisitiza zaidi mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo amesema kazi ya viongozi ni kusimamia sheria na taratibu za kazi,hivyo ataendelea kusimamia  sheria za utumishi wa umma katika halmshauri yake kwani mpaka sasa hali imeanza kubadilika kwa watumishi kuwa na nidhani.

Aidha, amesema halmshauri ipo tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa mkoa na kuhakikisha halmashauri yake haitapata tena hati ya mashaka kwa miaka inayokuja.

Gambo yupo katika ziara ya siku 3 wilayani Longido ambapo atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa katika wilaya hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Longido alipokuwa akuzungumzia hoja za CAG.


Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo akimchukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada ya kutoa maelekezo ya namna ya kujibu hoja za CAG


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, akisoma baadhi ya hoja zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) katika kikao chake na watumishi wa halmashauri ya Longido.





Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO