Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA KUACHANA NA MIGOGORO

 

Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea katika uchaguzi Mkuu wa nchi.

Athari za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto kwa jamii na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama na kupoteza sifa za usajili.

Hivi sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na kushiriki shughuli za chama.

Mojawapo ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro.

Mojawapo ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na kanuni za chama.

Hivyo natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake.

Pia kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.

 

 

 

CREDIT: BUKOBAWADAU

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO