Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mke wa Mfanyabiashara Mkubwa Arusha Afariki katika Ajali Mbaya Kikatiti

Mama mmoja anayeelezwa kuwa mke wa mfanyabiashara na mmiliki wa Aquiline Hotel ya Jijini Arusha bwa Charles Makoi, amefariki dunia katika ajali mbaya ya barabarani maeneo ya Kikatiti.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo mama huyu amefariki pamoja na wifi yake aliyetambulishwa kama Jamhuri Makoi. Walikuwa pia na mtoto mdogo ambaye amenusurika kifo lakini amejeruhiwa vibaya.

Msiba upo maeneo ya Sakina. Bado chanzo halisi cha ajali hiyo iliyohusisha basi la abiria hakijaweza kujulikana. Mashuhuda na waokoaji wanadai kukuta chupa za pombe ndani ya gari hilo.

Mungu Azilaze Roho za Marehemu Mahali Pema Amina!!

ajali
 

Marehemu enzi za uhai wake

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO