Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa Kwanza Maganga Lorry wa shule ya msingi Mbaaseny ,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali. Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akizungumza katika utoaji wa tuzo za Walimu Bora ,,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa 5 Mwalimu Clara Ernest wa shule ya Msingi Tuvaila ,
katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali. washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali. washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali. Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akizungumza na walimu katika Halfa ya Utoaji tuzo za walimu bora kwa walimu wa shule za msingi wilaya ya Meru zilizofanyika jana ,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali. washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Serikali
imetakiwa kuboresha mazingira bora ya walimu ili kukuza na kuboresha kiwango
cha elimu nchini kwani walimu ni kiungo muhimu katika elimu ambacho kinapaswa
kupewa kipaumbele kwenye kutimiza azma ya serikali kutoa elimu bora kwa
Watanzania.
Mkurugenzi
wa Shirika lisilokua la kiserikali la
The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa
Queyquen ameyasema hayo jana wakati wa utoaji wa tuzo za walimu bora wa shule
za msingi za serikali kwa kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu
nchini na ustawi bora wa jamii .
Melisa
alisema kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanategemea ubora wa elimu
waliyonayo watu wake hivyo ni vyema serikali inapofikiria kuboresha elimu
ifikirie kuboresha mazingira ya walimu kuanzia kitaaluma wanapoandaliwa kwenda
kufundisha ,vifaa vya kufindishia pamoja na stahiki zao.
“Bila Walimu Bora hakuna Elimu Bora ,Tumeamua
kuwatia moyo wa walimu kwa kutoa tuzo hizi na vyeti vya kutambua mchango wao
,washindi ni 10 mshindi wa kwanza amepatiwa cheti na shilingi la kitano,na
washindi wengine tumewapatia vyeti na fedha taslimu” Alisema Melisa
Afisa Elimu
wa Shule za Msingi Wilaya ya Meru Tumsifu Mushi
amewataka walimu kufanya kazi ya ualimu kwa moyo na kwa kujituma huku
wakitambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuandaa wataalamu watakaoisaidia jamii,taifa
na duni jukumu ambalo ni nyeti linapaswa kubebwa kwa uzito unaostahili.
Kwa upande
wao walimu waliopewa tuzo hizo Rose Salim wa shule ya Msingi Uraki na Ekaeli
Newasha wa Shule ya msingi Kimundo wamesema kuwa kundi la walimu limekua
likisahaulika mchango wake katika jamii hivyo tuzo hizo Zimeamsha ari na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.
“Kazi ya
ualimu unapaswa uwe unapenda watoto
unapenda kuwasaidia waweze kufika mbali kitaaluma ,binafsi nimefanya
kazi hii kwa miaka mingi na ninaipenda sana” Alisema Mwalimu Rose Salim
0 maoni:
Post a Comment