Baadhi ya washiriki katika mkutano wa maendeleo ya mkoa (RCC)wa Arusha kama wanavyonekana pichani. |
Aliyeshika kipaza sauti ni mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli akiwa anachangia mada katika mkutano huo wa( RCC)mkoani Arusha. |
Na.Vero Ignatus Arusha.
Jamii za wafugaji katika mkoa wa Arusha wameshauriwa kubadili mfumo wao wa maisha ili kutojikaribishia baa la njaa litakaloathiri ustawi wa jamii zao.
Hayo
yameelezwa na washiriki mbalimbali ambao wamehudhuria kikao
cha Ushauri wa Mkoa (RCC) ambacho
kimewashirikisha wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Arusha pamoja na
wakurugenzi.
Akichangia
mada mkuu wa wilaya ya Longido bwana Daniel Chongolo amesema jamii ya
wafugaji wamekariri katika wilaya wilaya hiyo,chakula
kilichopo nimahindi ambapo wangeliweza
kutojishughulisha kutafuta vyakula vingine kama viazi, mtama na ndizi ambazo
vinapatikana kwa wingi kwenye minada hasa ile ya Nanja na
Selela.
Pia
ameshauri jamii za wafugaji kua na utaratibu wa kujiwekea akiba ya chakula hasa
wakati ule bei ya mifugo iko juu kwani wanaweza kuuza sehemu ya mifugo yao na
kununua chakula cha kutosha na kuhifadhi katika maghala ya umma
yaliyopo wilayani
humo.
Hoja hiyo
imeonekana ikichangiwa na wakuu wa wilaya zingine ambapo mkuu wa
wilaya ya Ngorongoro
amesema katika utafiti aliofanya katika wilaya yake kwenye minada
mbalimbali bei ya
mahindi imepanda kutofautisha na vyakula kama ndizi na viazi, kwakua jamii hizi
hazina mazoea ya kula vyakula basi hulalamika ya kwamba kuna baa la
njaa.
Akichangia
mjadala huo mkuu wa mkoa wa Arusha amewataka wadau hao wa mkoa kuwa huru
kuchangia, kushauri na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika mkoa
wao.
0 maoni:
Post a Comment