Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HABARI MPYA*: Serikali ya Kenya Imewafukuza Kazi Wauguzi 25,000 Waliogoma kwa Kushindwa Kurudi Kazini.


Msemaji wa serikali ya Kenya, Alfred Mutua ametoa wito kwa watu wenye taaluma ya afya wote ambao hawana ajira au waliostaafu kufika hosiptali za umma kwa ajili ya kuajiriwa siku ya Ijumaa.

Wafanyakazi wa umma ambao wengi ni manesi waligoma tangu wiki iliyopita wakitaka kupandishiwa mishahara, marupupurupu na kuboreshewa mazingira ya kazi.

Vyama vya wafanyakazi wamepuuzia hatua hiyo wakisema ni mbinu ya kuwataka wajadiliane.
"Huu ni mchezo wa paka na panya, huwezi kuwafuta kazi wafanyakazi wote. Ni mbinuyaotu ya kutufanya haraka turudi kazini lakini mgomo wetu unaendelea mpaka madai yetu," Shirika la habari la Reuters limemnukuu Alex Orina, msemaji wa Taasisi ya wanataaluma wa afya akisema.

Alisema kwa wastani mfanyakazi wa sekta ya afya anapata kiasi cha shilingi 25,000 zaKenya($300, £190) kwa mwezi kwenye mshahara wake na posho.
Lakini Bw Mutua alisema wafanyakazi wa afya ‘hawaufuata maadili’ kwa kutorejea kwenyw majukumuyao.

Alisema majina yao yameondolewa katika orodha ya wafanyakazi wanaolipwa mshahara na si ‘waajiriwa wa serikali tena’, Dr Victor Ng'ani, mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Afya, wafamasia na wataalam wa meno alisema ulikuwa ni uamuzi wa ‘kizembe.’
Alisemaitakuwa vigumu kuwapata wafanyakazi mbadala kuziba nafasi ya miaka mingi ya watu wenye uzoefu na ujuzi wa kazi maalum.

Chanzo: BBC
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

7 maoni:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hapo kibembe! Watapata wale watakaofukuzwa huku bongo!

SeriaJr said...

ha haaaa Binadamu WOte (waafrika ) ni Sawa na Afrika ni Moja

Kiu ya Haki said...

Wanaweza kufanya lolote Kwakuwa Waziri Mkuu alisema Tumejipanga vizuri kukabiliana nao.

SeriaJr said...

tuombe Mungu aweke mkono wake hapo...
nahisi dalili ya nchi kuparaganyika kizembe kabisa..

Kiu ya Haki said...

Uwalimu wito/ Udaktari nao ni Wito, vip kuhusu Urais na Uwaziri mkuu nao ni wito au sio Wito.

Kiu ya Haki said...

Uwalimu wito/ Udaktari nao ni Wito, vip kuhusu Urais na Uwaziri mkuu nao ni wito au sio Wito.

SeriaJr said...

hata uwaziri, urais nao ni wito...
siamini kama kuna kazi ya akili isiyokuwa na wito hasa kama ni kwa maslahi ya wengine..

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO