Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litatumia fursa ya tukio la kupatwa kwa jua kama njia mojawapo ya kutangaza hifadhi za taifa hususani zinazopatikana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Magharibi mwa Tanzania.
Tukio la kupatwa kwa jua linataraji kuonekana vizuri ukilinganisha na maeneo mengine Duniani katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani hapa,eneo ambalo liko jirani na Hifadhi za taifa za Ruaha,Kitulo na Katavi.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete
alisema maandalizi kwa ajili ya kupokea wageni wanao tarajia kufika
nchini kwa ajili ya tukio hilo ambalo limekuwa likitokea kwa nadra.
“ Wataaam na wanasayansi wa
kitaifa na kimataifa wathibitisha kuwa eneo pekee ambalo tukio hilo
litaonekana vizuri kuliko maeneo yote duniani ni Tanzania katika mikoa ya
nyanda za juu kusini,eneo ambalo lina vivutio utalii vinavyopatikana katika
hifadhi zetu za Katavi.Kitulo na Ruaha”alisema Shelutete .
“Shirika limejipanga kuhakikisha kuwa wageni wanoukuja kwa ajili ya tukio hilo pia wanapata fursa ya kuingia katika moja ya hifadhi zetu,niwaomba wadau wa sekta ya utalii nchini kutumia nafasi hii adhimu kukutana na wageni wanaokuja ili kuuza bidhaa zao za utalii”aliongeza Shelutete.
Naye mkuu wa hifadhi ya taifa ya
Ruaha Christopher Timbuka alisema kituo kikubwa ambacho kimethibitishwa
kutumika kwa ajili ya watu kujionea vizuri tukio hilo ni katika eneo la rujewa
wilaya ya mbarali ambako maandalizi yote muhimu yamefanyika.
Kwa upande wake mhifadhi wa idara
ya utalii Tutindaga Mdoe alisema baada ya tarifa za tukio hilo
kuthibitishwa idadi ya wageni imeanza kuongezeka na kwamba wameandaa mahema na
eneo la vyakula na vinywaji kwa wageni watakaofika kushuhudia tukio hilo katika
eneo la Bonde la Ihefu lililopo katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti
hili katika eneo hilo maarufu kwa kilimo cha mpunga umebaini asilimia kubwa ya
nyumba za kulala wageni tayari zimejaa kwa tarehe ya tukio hilo.
Mwisho.
0 maoni:
Post a Comment