Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa aliekuwa Waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Adam Clement Mwakajuki (pichani) amefariki dunia leo alarisi na taratibu za kusafirisha mwili wake kwenda Zanzibar zinaendelea.
Brigedia Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam leo alaasiri baada ya kuugua kwa mfupi. Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na kitu gani lakini alifikishwa hospitalini mapema wiki hii.
Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 kupitia chama cha Afro Shiraz (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa Kilimo na Mifugo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ.
Brigedia mstaafu Adam Mwakanjuki amewahi pia kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa muda mrefu.
Blog hii inatoa pole kwa wafiwa wote, Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema, Amina!
CHANZO: TBC
0 maoni:
Post a Comment