Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Sababu za Joseph Mbilinyi (Sugu) kukamatwa na kuachiwa na Polisi jana

150Kuhusu Joseph Mbilinyi 'Sugu', Mbunge wa Mbeya Mjini. Ni kweli alikuwa polisi Dodoma, alikoitwa kwa madai ya kutoa lugha ya matusi kwa Ndugu Mizengo Pinda, lakini hajaandikisha maelezo, kwa sababu 3, zifuatazo:

1. Wakili wake, Tundu Lissu, amewaambia kuwa Polisi hawawezi kumkamata na kumhoji Mbunge Sugu, iwe ukumbini, maeneo ya bunge, au nje ya maeneo ya bunge, wakati bunge likiendelea, kutokana na parliamentary immunity aliyonayo hadi polisi watakapofuata taratibu zinazotakiwa.

2. Neno hilo wanalotuhumu kuwa ni lugha ya matusi, si tusi kwa sheria za nchi yetu, bali linaweza kutumika kwa vitu au mtu anayefanya matendo au kusema maneno yanayostahili kuitwa hivyo.

3. Wakili wake (Tundu Lissu)kawauliza, nani mlalamikaji katika tuhuma hizo, je wamepokea malalamiko ya Ndugu Pinda mwenyewe? Majibu yalikuwa ya kigugumizi"

Wameondoka polisi kwa makubaliano ya kurudi kesho asubuhi.

Na: Tumaini Makene, Afisa Habari Chadema.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO