Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Waziri Mwijage azindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka kijijini Maisha Plus


WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa nchini Tanzania Mhe. Charles Mwijage leo amezindua rasmi mashine ya kusaga na kukoboa nafaka katika kijiji cha Maisha Plus. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo Mhe. Mwijage alisema kitendo cha washiriki hao 16 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki kuweza kubuni mashine ni sawa na kufaulu mitihani mikubwa ya kimaisha. Alisema mashine hiyo ni mkombozi kwa watu wote wa Afrika Mashariki kwa sababu inaweza kusaga bila kutumia umeme lakini pia inamuwezesha mtu kufanya mazoezi. 2016-10-30-PHOTO-00000145 “Hii mashine ni njia mbadala ya kumuwezesha mtu kufanya mazoezi badala ya kwenda gym kufanya mazoezi utaweza kutumia mashine hii ukiwa unasaga nafaka huku unafanya mazoezi,” alisema Mwijage. 2016-10-30-PHOTO-00000148 Alisema ni vyema kwa washiriki kutumia njia hiyo kuweza kubuni mashine nyingine zaidi ili kuweza kuongeza soko la Afrika Mashariki.
Alitoa wito kwa mshiriki atakayeshinda Tzshs. Milioni 30 za Maisha Plus aziwekeze katika uchumi wa viwanda. 2016-10-30-PHOTO-00000147 Grace PEMBA kutoka Mtwara aula Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane. "Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho."
Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi. Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter. Maisha Plus inaratibiwa na kampuni ya DMB na vipindi kutengenezwa na kampuni za True Vision Productions, KP Media na Pumzika Communications. #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO