Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWALIMU ATEKWA, AFANYIWA UKATILI JIJINI ARUSHA, POLISI WAMUOKOA


MWALIMU aliyejitambulisha kwa jina la Batuli Isaya wa Shule ya msingi Unga Ltd (pichani) amekaririwa kwenye audio inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa alitekwa na watu wasiojulikana na kisha kutelekezwa mahali akiwa hajitambui mpaka alipokuja kuokotwana askari Polisi na kujikuta yuko Hospitali ya Mt meru akitibiwa. Tukio hilo limefunguliwa jalad namba AR/RB/12730/2016katika kituo kikuu cha Polisi Arushana kwamba upelelezi bado unaendelea. Kisa kizima kama kilivyosimuliwa kwenye audio hiyo ni hiki hapa.. Bofya hapakupata link yenye Audio halisi

"Kwa majina naitwa Batuli Hamad Isaya, ni Mwalimu wa Shule  ya Msingi Unga Ltd, Kata ya Unga Ltd Mkoani Arusha. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatatu tarehe 3 jioni mida ya saa  moja, nilikuwa naenda  dukani  kununua vocha simu  yangu ilikata. Kwa hiyo nikachukua hela nikaenda dukani  kununua vocha ambapo  ni barabarani. Nimefika barabarani nikanunua vocha nikaikwangua nikawa narudi nyumbani. Kutoka barabarani mpaka nyumbani  kwangu kuna uchochoro ambao ni nimrefu kidogo, nikawa nikitembea kuelekea nyumbani huku naingiza vocha kwenye simu, namulika namba naingiza, namulika namba naingiza.

Mwalimu Batuli aliyefikwa na maswaibu hayo akiendelea na matibabu

Mpaka saa  tisa na nusu, sikuona chochote, baadae tena nikapigiwa simu,  unaitwa Ofisi za Elimu. Nikarudi tena Ofisi za Jiji. Nilivyofika nikakutana na barua Afisa Elimu amenipa barua ya kutengua uteuzi wangu. Nikaipokea ile barua pale pale nikaifungua nikaisoma imeandikwa Kutengua Uteuzi wa Kuwa Mratibu wa Elimu Kata ya Ngarenaro. Nilipoisoma tena, kwanza nikashtuka, nikatetemeka, nikasema nimefanya nini? Ni nini nimeshindwa? Sikupata majibu sahihi, nikamuuliza Afisa Elimu hii barua ni vipi? Akasema mimi  sijui kinachotakiwa fuata maelekezo ya barua iliyokuelekeza, aliyekuteua ndio aliyekutengua.



Basi nikaipokea barua mara  moja nikarudi kituo cha kazi nikaripoti nikamuomba Mwalimu Mkuu wangu akanipangia vipindi nikaendelea na kazi. Lakini baada ya siku mbili, nilianza kujiuliza kichwani, hii nafasi ndogo nimepewa nimeshindwa kwasababu gani? Nikataka sababu zilizonisababisha  kushindwa hii kazi.

Nilichokifanya nilienda kwa Mkuu wa Wilaya ambaye  ni DC wangu, nikamuelezea kwamba, nikamshirikisha kulikoni kwamba  nimepata promotion ndani ya wiki nne  halafu wamenitengua lakini hawajanipa sababu za msingi na sielewi ni kitu gani ambacho nimekosea, napaswa kujua kwasababu Mimi nimejiendeleza, nina  skills, nina  uwezo wa kufanya kazi, sasa kama kazi kama hii ndogo nimeshindwa kufanya kazi kubwa nitawezaje na nimeshatuma application mbalimbali?



Kwakweli, Mkuu wa Wilaya akaniambia , akasoma zile barua, nikampa background kidogo ya kazi ambazo nimeshawahi kufanya, nimeshiriki kazi nyingi katika jamii, akanambia hii itakuwa ni sintofahamu, ananiambia hebu ziache hizo barua zako zote mbili nitafuatilia nijue kwa Mkurugenzi kuna sintofahamu gani. Baadae ikabidi  nimuelezee Mimi naona kama vile *Mkurugenzi wa Jiji la Arusha* Hajanitendea haki, kwasababu, kwanza alipaswa kuniambia ni kitu gani ambacho nimekosea, kitu gani ambacho nimeshindwa, yaani kipi ambacho sijakifanya mpaka aniandikie barua ya kunitengua? Lakini sikupata ushirikiano. Ushirikiano ni kwamba rudi kafanye kazi ukae kimya.

Sasa nikawa nahusianisha hii kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ndio imepelekea mimi  kuja  kufanyiwa  kitendo kama hiki nilichofanyiwa au ni kipi kilichosababisha? Sikupata majibu sahihi.
Barua ambayo mwalimu Batuli anaeleza ndiyo 'iliyomtumbua' bila kuelezwa sababu

Lakini baadae nikaendelea kuvuta kumbukumbu zangu ziku  za nyuma, nilivyopata hii barua ya promotion, katika haya maGrupu ya WhatsApp, ambayo niliona Mheshimiwa *Mbunge Catherine Magige alishawahi kuandika kwamba watashughulika na vyeo vyangu, watanishughulikia na wakasema kwamba hawaongei na mbwa wataongea na mwenye  mbwa* na hawakunisight kabisa jina  langu. Lakini nikafuatilia nikaona ni meseji ambazo hazina mantiki nikawa nimetulia.

Sasa baada ya kupata hili tukio la kutekwa ndio nimeanza kuhusianisha, *je, ni Mkurugenzi ndio kwasababu nimelalamika kwa Mkuu wa Wilaya ndio amesababisha hili au ni Mbunge Catherine Magige kwasababu ya kumuadvise katika kazi zake ameona namkosoa sana katika kazi zake ndogondogo?* Nimeshindwa kupata majibu.
Na mpaka kufikia sasa hivi naendelea na dawa  ambazo  zinanisababishia  kuharisha, kutapika na *Kesi hii iko Polisi kwasababu Polisi ndio  walioniokota.*


Polisi wameahidi watalishughulikia  lakini leo  nina  siku ya tisa  sijaona reaction yeyote na wameniahidi kwamba wanaendelea kufuatilia. Sasa sijajua wanafuatilia nini au sijajua ninasaidikaje kwasababu mpaka dakika hii sielewi lakini iko mikononi mwa  Polisi walishachukua maelezo, wamekuja kunitembelea, wanafuatilia. Na *hata RCO alikuja  hospitali kunisalimia* kwa hiyo bado wanafuatilia.

Kwa hiyo nilikuwa naiomba  Serikali kama itaweza  kunisaidia afya yangu niendelee kuchunguzwa kwasababu mpaka dakika hii *sina  uhakika kama sindano nilizochomwa ni kweli  ni hizo za insulin kwamba sukari ishuke au ni virusi  vya Ukimwi wameniingizia ili nife taratibu, au ni nini kimewekwa katika mwili wangu*, bado sijajiridhisha kwasababu sijachekiwa sumu  kwenye mkojo, sijachekiwa...yaani sielewi kwakweli.
Kwa hiyo ni ninaomba kwa yule ambaye  anaweza kunisaidia basi anisaidie.

Ripoti ya daktari kuhusu matibabu ya Mwalimu huyo
Naomba pia swala hili hata Mh Rais  aweze kulifahamu kama kuna mtendaji ambaye  anaweza kuenguliwa nafasi yake  pasipo kujua kosa lolote, ni vyema akalifahamu. Ikawa ni vizuri na Mimi nikaelewa kwamba nilichofanyiwa ni haki? Uko kwenye nafasi, hujawahi kufanya kosa lolote, hujakutwa na kashfa yeyote, hujahusika na watoto hewa au hujahusika na ubadhirifu wa fedha, umetenguliwa pasipo sababu ya msingi na kila ukihoji wanakwambia kwamba nyamaza kimya endelea kufanya kazi. Nashindwa kuelewa kwakweli, bado naona Mkurugenzi wangu wa Jiji la Arusha hajanitendea haki, labda kuna sintofahamu lakini ni vyema akaiweka wazi kwasababu naona kwanza amenichafulia faili  kutokana  na nina  uwezo wa kufanya kazi. Na kazi nafanya. 

Kwa hiyo kama kuna chombo cha sheria kinafuatilia kitende haki ..."
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO