Wafanyabiashara wacheni kuipigachenga Serikali kwa kutokulipa kodi
Raisi wa (FGBMFI)nchini Tanzania Injinia John Njau |
Na.Vero Ignatus
Arusha
Wito
umetolewa kwa jamii ili waweze kuwa na maisha bora wawe na shughuli za halali
za kufanya zitakazo waingizia kipato,ili wasiwe tegemezi katika familia zao na
jamii kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa na Jaggy Singh ambaye ni mkurugenzi mkuu wa
ushirika ( FGBMFI)wa
Kimataifa wa wafanyabiashara Wakristo,ambapo amewataka watu kufanya
shughuli zao katika misingi iliyo halali ,katika uadilifu na waepuke
udanganyifu.
Sigh
amesisitiza kuwa lengo kuu la mkutano ni kuwaleta wafayabiashara pamoja,
kubadilishana mawazo na changamoto wanazopitia,kuonyesha umuhimu wa kuishi
maisha ya uhalisia na kufanya kazi kwa bidii zaidi,ambapo amewataka kuepuka
udanganyifu wasiipige serikali chenga kwa kutokulipa kodi ,wafuate utaratibu na
sheria za nchi.
Kwa
upande wake raisi wa (FGBMFI) nchini Tanzania Injinia John
Njau amesema
ushirika huo wa wafanyabiashara wa Kimataifa hawajishughulishi na biashara peke
yake bali wanahubiri Injili kamili kwa kutoa ushuhuda wa vitendo hata kama
wafanyabiashara wengine hawaamini wao wanatimiza
wajibu.
Ameainisha
kuwa nchini Tanzania kwa sasa wana matawi ya ushirika huo wa
wafanyabiashara Wakristo
yapo(7) ambayo ni kama ifuatavyo,
Mbeya,Mwaza,Shinyanga,Kilimanjaro,Arusha,Dar
es-salaam,Manyara pamoja na Zanzibar ,na kwa upande wa Kmataifa kwa ujumla yapo
169,ambapo kila tawi linafanya kazi kutokana na taaluma walizo
nazo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo John
Majo ,ambaye
pia ni mwenyekiti wa tawi la Arusha ,amesema kuwa ushirika huo wa
wafanyabiashara wa Kikristo mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga maadamu
anajishughulisha ,awe ameajiriwa ,mfanyabiashara ,au mjasiriamali anaruhusiwa
nia yao kuu ni kuwaleta pamoja ili wamjue Mungu zaidi
pia.
Aidha
amewataka vijana wa kiume wasipende maisha ya urahisi ya bali wachape kazi
kwabidii,wajitume waache tabia mbaya ya kuwa tegemezi kwani wananguvu Mungu
amewapa wazitumie ili kujiingizia kipato kwani itawajengea heshima
katika jamii
“Unamkuta
kijana yupo tu mtaani hataki kujishughulisha ukimtazama hana ulemavu wowote
,anapenda maisha ya kifahari nay a starehe lakini kazi hataki kufanya matokeo
yake anajikuta amejiingiza kwenye mambo ya aibu na fedheha kubwa katika
jamiii,inatuhuzunisha sana sisi kama wazazi badilikeni mjitume “alisisitiza
John.
w
Wito umetolewa kwa jamii ili waweze kuwa na maisha
bora wawe shughuli za halali za kufanya
Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi mkuu
wa Ushirika wa wafanyabiashara wa Kimataifa wa Kikristo hapa nchini
Jaggy Sigh akiwa na wajumbe wengine waliohudhuria katika kongamano
hilo la siku tatu lililofanyika katika Hotel ya Corrido Sprigs iliyopo
Jijini Arusha.picha na Vero Ignatus.
Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya kongamano hilo ambaye pia ni mwenyekiti wa Tawi la Arusha John Majo.Picha na Vero Ignatus.
|
0 maoni:
Post a Comment