mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiongea na waandishi wa habari mara baada ya maamuzi ya ruf
aa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la longine Onesmo Nangole
Na Woinde Shizza,Arusha
Mahakama ya
rufaa kanda ya Arusha imeshindwa kutoa maamuzi ya rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido
,Onesmo Nangole(CHADEMA) ambaye anapinga maamuzi ya mahakama kuu iliyomvua ubunge
wake, badala yake imeagiza mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi mkuu wa
uchaguzi katika jimbo hilo aunganishwe katika shauri hilo.
Aidha
mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa mrufani kwa ajili ya kufanya marekebisho ya
notisi yake ya rufaa na kuyaleta mahakamani hapo ili msimamizi wa uchaguzi
pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali waingizwe kama mashaidi muhimu katika rufaa.
Akisoma
taarifa ya majaji watatu walikuwa wakisikiliza rufaa hiyo mahakamani hapo
Msajili wa mahakama rufaa John Kayanza alisema kuwa mahakama ya rufaa aitatenda
haki katika hukumu yake iwapo haita msikiliza mwanasheria wa serikali pamoja na
msimamizi wa uchaguzi jimbo la Longido na imewataja kama mashaidi muhimu kwa
upande wa mrufani
“kama
mahakama itatoa uamuzi bila kusikiliza mwanasheria wa serikali na msimamizi wa
uchaguzi haitakuwa imetenda haki katika
mahamuzi hivyo mahakama imeonelea ni vizuri
mrifani akaifanyie marekebisho notisi yake na ndani ya siku 21
aiwasilishe mahakamani”alisema Kayanza
Katika rufaa
hiyo mrufani Onesmo Nangole aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido alikata rufaa
kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo ilitengua
ubunge wake na kuagiza msimamizi wa
uchaguzi atangaze jimbo hilo kuwa lipo wazi.
Katika kesi
hiyo Onesmo Nangole( CHADEMA) anawakilishwa na mawakili wawili ambao ni Methodi kimomogoro akisaidia na wakili John
Materu ambapo kwa upande wa warufaniwa Dkt.Steven Kiruswa (CCM) anawakilishwa
na mawakili watatu wakiongozwa na DKT.Masumbuko Lamwai akisaidiwa na Daudi
Haraka pamoja na Edmond Ngemela.
Rufaa hiyo inasikilizwa na Majaji watatu ambao ni jaji Sauda Mjasiri,Jaji
Musa Kipenka pamoja na Profesa Ibrahimu Juma.
Akiongea
mara baada ya kesi hiyo kuairishwa Onesmo Nangole alisema kuwa anaishukuru
mahakama kwa kuwapa nafasi na kuona umuimu wa mwanasheria wa serikali pamoja na
msimamizi wa uchaguzi wilayani longodo kuja kutoa ushaidi katika shauri hilo na
anaamini mahakama hiyo itamtendea haki.
Kwa upande
wa Dkt,Kiruswa (CCM) alisema yeye atatizo na maamuzi ya mahakama na anaiachia
mahakama iendelee kushulikia shauri hilo na anaamini itatenda haki.
0 maoni:
Post a Comment