Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAFANYAKAZI WA NMB,TAWI LA NELSON MANDELA WATOA MSAADA NA ZAWADI KWA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI


Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface akitoa maelzo mafupi kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela waliofika hosptalini hapo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wagonjwa pamoja na msada wa vitendea kazi vya kufanyia usafi kwa hospitali ya Mawenzi.
Wafanakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakishusha zawadi mbalimbali kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi.
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akimueleza jambo Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitai ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface walipofika hospitalini hapo kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface akieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela walipotembelea wagonjwa na kuwapa zawadi.
Meneja wa Benki ya Nmb tawi la Nelson Mandela mjini Moshi,Emanuel Kishosha akikabidhi msaada wa vitendea kazi kwa ajili ya usafi kwa kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi Dkt Josephat Boniface.
Baadhi ya Washauri wa Afya kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na watumishi wa hospitali hiyo wakishuhudi tukio la kukabidhi msaada huo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa hosptali ya Rufaa ya Mawenzi.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa mbalimbali kwa ajili ya kufanyia usafi katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela wakitoa zawadi mbalimbali zikiwemo Sabuni za kufulia,sabuni za kuogea ,dawa za meno,maji ya kunywa na vingine vingi kwa wagonjwa waliolazwa kati wodi mbalimbali hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mawenzi.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela,Emanuel Kishosha akiwa amebeba maji kwa ajili ya kugawa katika wodi ya watoto hspitalini hapo.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi ,Dkt Josephat Boniface akifurahia jambo na mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya nmb tawi la Nelson Mandela.
Wagonjwa wakipewa zawadi kutoka kwa wafanyakaz wa benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi.
Kaimu Mganga Mafwidhi wa Hspitali ya rufaa ya mkoa ,Mawenzi Dkt Josephat Boniface akitoa neno la shukurani kwa wafanyakazi wa benki waliofika kutoa msaada pamoja na zawadi kwa wagonjwa katika hospitali hiyo. 
Kaimu Mganga Mafwidhi wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi Dkt Josephat Boniface akipeana mikono na wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi mara baada ya kukabidhi msaada pamoja na zawadi kwa wagonjwa. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO