Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MTEULE DKT. WILBROD SLAA PIA AKUTANA NA MAAFISA WAKUU WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WANAOTARAJIWA KUSTAAFU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael Isamuhyo watatu kutoka (kulia) Brigedia Jenerali Aron Robert Lukyaa wapili kutoka (kulia), Kanali Peter Samuel Sameji wa kwanza (kulia).  Wengine katika picha ni Brigedia Jenerali William Ephraim Kivuyo wapili kutoka kushoto na Brigedia Jenerali Elizaphani Lutende Marembo. PICHA NA IKULU

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO