Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Alphonce Mawazo Meneja Kampeni wa Mgombea wa Chadema Kalenga, Achukua Nafasi ya Lema


Alphonce Mawazo, Kamanda wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Picha na Arusha Times)

Arusha255 inaweza kuthibitisha uteuzi mpya wa Ndugu Alphonce Mawazo kama meneja kampeni za kumnadi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi Grace Tengega Mvanga katika uchaguzi mdogo wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Machi 16, 2014 katika Jimbo la Kelenga Mkoani Iringa kwa lengo la kumpata mbunge atakayewakilisha wana Kalenga baada ya kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Marehemu Dr Mgimwa, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha.

Awali alikuwa ameteuliwa Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema kuwa meneja kampeni, lakini kutokana na majukumu ya Bunge la Katiba imeonekana hatakuwa na muda wa kutosha kufanya kazi hiyo.

Alphonce Mawazo (kushoto) na Gobless Lema latika moja ta tukio la kisiasa.  Hapa chini ni maelezo binafsi ya Mawazo kufuatia uteuzi huo kama alivyoandika kwenye ukufasa wake wa Facebook

“Nakishukuru chama changu cha chadema kwa kuniamini na kunipa heshima kuu ya kuwa kampeni meneja wa hapa Kalenga panapofanyika uchaguzi mdogo wa ubunge baada kifo cha aliyekuwa Mbunge Wa jimbo hili Dr. Mugimwa.

Mikoba hii nimeirithi kutoka kwa Mh: Lema Mbunge wa Arusha Mjini kutokana na wabunge kushiriki moja kwa moja kwenye Bunge la Katiba hivyo kuwa na muda mfinyu sana aa kufanya shughuli zingine nje ya Bunge.

Natambua sio kazi ndogo na wala sio mteremko.  Ninchoweza kuwaahidi ni mapambano yasiyo na simile. Dhamira yangu ni dhabiti mno, utayari wangu kutimiza adhima ya mioyo ya watanzania na ile ya chama changu haipimiki. Hakuna gharama itakayo kuwa ngumu kwangu kuilipa kwa ajili ya ukombozi wa taifa langu, nina maanisha HAKUNA. Nitajie gharama yoyote nitakuambia am ready to pay ili mradi niwe na uhakika ya kwamba kama ni damu yangu inatakiwa haimwagiki bure kwa faida ya wachache.

Namwamini Benson Kigaila ambaye ni operation kamanda, Mimi humwita General wa vita. Namwamini Dr:slaa kipenzi cha watanzania na MTU shupavu sana. Namwamini Mbowe Mwenyekiti ambaye ni chachu kubwa ya mabadiliko Tanzania na inspirational kwa vijana. Naiamini Kamati Kuu ya Chadema.

Nilipokea kwa mshituko kidogo taarifa za wasaliti wawili kule Shinyaga lakini baada ya kusikia majina yao nikapumua maana nawafahamu fika na kwa wakati mmoja nilishawahi kuwaonya kuwa chama kingewashinda. Yametimia, sina sikitiko hata chembe waacheni waondoke lilikuwa bomu hatari sana. Nimemwambia Dr Slaa asipoteze muda kuwafikiri. Kkwa mila za kiafrika hatuombolezei mimba iliyo haribika.

Mwisho naomba mtuombee sisi tulioko vitani Kalenga, vijana wenu wengi wamejitoa na wako huku, wengi wao wamekuja kwa kusukumwa na matamanio ya mabadiliko na hawajui watakula au kunywa nini. Kama una chochote waweza kutuma kupitia namba yangu 0756039703 au kama unamjua yoyote aliyeko field huku tafadhali msaidie. ALUTA CONTINUA.”
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO