Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya Tigo Kanda ya
Kaskazini George Lugata Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya
Udhamini wa Mashindano ya Kilimanjaro International Marathon
Wateja wakifurahia huduma za Tigo zilizoboreshwa katika Ofisi za Tigo zilizoko Blue Rock jijini Arusha
Na Woinde Shizza,Arusha.
Kampuni ya
Simu za mkononi ya TIGO imejipanga kunogesha mashindano ya Kilimanjaro
International Marathon kupitia udhamini mnono ya mashindano hayo kwa upande wa
kilomita 21 ambapo licha ya udhamini huo watahakikisha huduma zote muhimu za
kifedha zinapatikana katika mashindano hayo.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini,George Lugata amesema kuwa zaidi ya nchi 45 zinatarajia
kushiriki katika mashindano hayo ya kimataifa yanayotarajia kufanyika Februari
26 mwaka huu mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro.
George
alisema kuwa kampuni ya Tigo imejipanga kuhakikisha kuwa huduma za Tigo Pesa
zinapatikana kwa kipindi chote kwani wameongeza idadi kubwa ya mawakala wataotoa huduma hizo.
“Ni vyema
tukatambua kuwa wateja kutoka mitandao yote nchini wanaweza pia kulipia huduma
na bidhaa kutoka katika maduka ya wafanyabiashara wowote jijini Moshi kwenye
mabango yaliyoandikwa Lipa kwa Tigopesa” Alisema George
Alisema kuwa
katika kipindi chote hicho watatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu ili
kuhakikisha kuwa wa Washiriki na Watakaohudhuria wanafurahia huduma hizo.
Mkurugenzi
huyo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kushiriki mbio
hizo zenye hadhi kubwa kitaifa na kimataifa .
0 maoni:
Post a Comment