Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RC GAMBO AINGILIA KATI SAKATA LA MATUMIZI YA ARDHI KWA WANANCHI WA SEKELA-MONDULI


Na,Vero Ignatus,Monduli
 Ziara ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo katika vijiji vya Mbaashi na Selela amekumbana na mgogoro wa matumizi ya ardhi katika kijiji cha Selela ambapo wananchi wamemweleza kuwa halmashauri ya kijiji hicho imetoa sehemu ya eneo la shule ambalo lilikua ni kiwanja cha mpita na kulifanya kuwa soko ilhali kiwanja cha michezo kuhamishiwa sehemu ingine.

Hayo yaliibuka baada ya mkuu wa mkoa Mh Gambo kupokea maswali na kero za wananchi ambapo wananchi wengi walionyesha kutoridhishwa na maamuzi mengi yaliyofanywa na halmashauri ya kijiji hicho juu ya matumizi yenye manufaa ya ardhi.

Mh. Gambo ameitaka halmashauri ya kijiji hicho kurudisha eneo la michezo eneo la shule na soko lipelekwe mbali na maeneo hayo ya shule ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi. 
Pia amemtaka afisa elimu msingi Bi Theresia Kyara na mdhibiti ubora wa shule kufika shuleni hapo na kijiji cha Nadosoito ili kuwaelekeza wanakijiji juu ya ubora wa shule zinazotakiwa na serikali kwani halmashauri ya kijiji cha Nadosoito kipo katika hatua za awali za ujenzi wa shule ya msingi.

Mh Gambo alipokea lalamiko la Mlemavu  Aloyce Mollel kuwa kwa miaka Zaidi ya saba amekua anaomba halmashauri ya kijiji cha Selela impatie eneo la kuishi na mpaka sasa ameshaandika barua zaidi ya kumi na saba bila majibu
Katika hali isiyo ya kawaida Mh Gambo alimwita mwenyekiti wa kijiji na Afisa Ardhi wa halmashauri ya Monduli Bw. Adili Mwanga ambapo kwa pamoja waliamua ndani ya wiki tatu watakua wamemaliza kupima ardhi ya kijiji hicho na watakua tayari kwa  kuviuza kwa wananchi, Mh Gambo aliamua kumlipia kabisa mlemavu huyo kiasi cha shilingi Laki moja na nusu ikiwa ni gharama ya kiwanja kimoja kama makisio ya gharama yalivyotolewa na mtaalamu huyo wa ardhi.

Naye mbunge wa Monduli Mh Julius Kallanga Laizer amemshukuru sana mkuu huyo wa mkoa kwa namna anavyopambana kutatua kero za wananchi wa Arusha na anaishukuru sana serikali ya Mh Dr John Pombe Magufuli kwani utekelezaji wa ilani ya CCM unaonekana kutoa majawabu kwa matatizo mengi ya wananchi.

Wilaya ya Monduli ina jumla ya migogoro ya ardhi mikubwa mitano (5). Migogoro mitatu inahusu mipaka ya wilaya ya Arumeru na Monduli,wilaya ya Babati na Monduli na wilaya ya Longido na Monduli. Migogoro hii ipo katika hatua nzuri ya utatuzi kwa kushirikiana na Ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Arusha.

Toka awamu ya tano imeingia madarakani kumekua na mchakato wa kufuta mashamba pori ambayo kwa muda mrefu yamekua hayaendelezwi. Ikiwa hadi sasa mashamba 31 yameshafutiwa umiliki 13 na Rais wa Jamhuri ya Muungano na 18 kwa ngazi ya kijiji.
Image
Mkuu wa mkoa akifungua nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mbaash
ImageImage
Mkuu wa mkoa Mh Gambo akikabidhi mchango wake wa shilingi laki tano kwa diwani wa kata ya Selela ikiwa ni mchango wake katika kituo cha Afya Selela
Image
Image
Wanafunzi shule ya msingi Selela wakimkaribisha mkuu wa mkoa shuleni kwao
Image
Mh Gambo akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya waalimu na madara mawili
Image
Image
Mh Gambo akipokea zawadi toka kwa wananchi wa Selela
Image
Kutoka Kushoto ni mbunge wa Monduli Mh Julius Kallanga, Mh Mrisho Gambo na mwisho ni Diwani kata ya Selela bwana Cuthbert Meena wakijadili jambo
Image
Baadhi ya wananchi kata ya Selela wakimsikiliza Mh Gambo katika mkutano wa hadhara
Image
Bi Namnyaki Lekule akitoa kero yake kwenye mkutano
Image
Bwana Aloyce Mollel akipokea fedha taslimu shilingi laki moja nusu ikiwa ni mchango wa kumnunulia kijana huyo kiwanja
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO