Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nafasi 30 za Kazi Kwa Askari Wasaidizi wa Jiji la Arusha

Halamashauri ya Jiji la  Arusha imetangaza nafasi 30 za ajira kwa askari wasaidizi wa Jiji ambao watapatiwa mafunzo ya uongozi na crowd management kwa muda wa miezi 4 ili kuweza kuwahudumia wananchi bila kuwanyanyasa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu katika kituo cha Redio 5 cha Jijini hapa mapema leo  asubuhi, Mstahiki Meya wa Jiji, Mh Kalisti Lazaro amesema Halmashauri imeamua hivyo ili kuondoa kero iliyokuwepo ya mgambo wa Jiji ambao amedai imechangiwa na kuwa vibarua tu wa Jiji.

Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hizo ni tarehe 20 January 2016 ambapo sifa stahiki zimeelekezwa kwenye tangazo hili hapa.

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Anonymous said...

Enter your comment...duh mtu na degree take akapige mgambo

Anonymous said...

kazi kweli kweli

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO