Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema amesema kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salam Makonda anajua aliko Ben saanane hivyo awajibike kumleta.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana jijini Arusha Lema alisema jeshi la polisi ndio lenye dhamana ya kufanya uchunguzi wa kina katika matukio ya watu kupotea na siyo mkuu wa mkoa.
Aidha Lema alisema kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutoa tamko la kuhakikisha kupatikana kwa Msanii Roma Mkatoliki kabla ya jumapili kimedhihirisha wazi kuwa anahusika na kutekwa kwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Beni Saanane.
"Watawala wanajua alipo Beni Saanane kama ambavyo makonda alijua alipo Roma Mkatoliki tunataka watuletee akiwa hai ama akiwa amekufa watuletee mifupa yake" alisema Lema.
Alisema Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekuwa msemaji wa nchi wakati maswala ya mtu kutekwa au kupotea alitakiwa kuzungumzia Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba jambo ambalo amekaa kimya.
"Siro alisikika akisema kuwa Roma Mkatoliki hayupo mikononi wa Polisi , wakati huo huo Mkuu wa mkoa akatoa tamko kuwa kabla ya Jumapili Roma atakuwa amepatikana ninani amempa mamlaka Mkuu huyo kuwa msemaji wa Polisi" alihoji Lema.
Alisema ni dhahiri kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ama ameshindwa kazi au anajua mambo yanakoendelea ila anahofia kukutwa na kilichomkuta aliyekuwa waziri wa habari,Utamaduni, Sanaa na michezo Nape Nnauye hivyo anaamua kunyamaza.
"Tuendako sasa mheshimiwa Rais ammpe Uwaziri wa mambo ya ndani Makonda maana amekuwa akiingilia jeshi la polisi katika utendaji wake jambo ambalo halimhusu" alisema.
Alisema ipo siku ambayo hawatakuwa chadema , CUF, au CCM wananchi hawa wanaoonewa watakataa kutekwa ambapo alisema inaweza kuleta machafuko nchini
Aliongeza kuwa yeye Mwenyewe anatembea kwa hofu ambapo alisema nchi haiko salama kutokana na matukio ya utekwaji yalivyoshamiri hii ikiwa inasababishwa na watu kutotakiwa kusema ukweli.
"Nimejipanga kuhamasisha maaandamano nchi nzima katika vyuo ya kutaka vijana waandamane kutafuta alipo Saanane, kuna wangapi wamepotea hatujui walipo tukiendelea kukaa kimya watatekwa wengi zaidi" alisema.
Aliongeza kuwa ni takribani miezi 6 tangu kukamatwa kwa Beni na hadi sasa Chama chao pamoja na wazazi wake hawajui alipo ambapo alisema taarifa walizozipata ni kuwa Makonda anajua alipo Saanane.
"Tunamtaka Makonda aseme Ben alipo la sivyo nchi inakwenda pabaya Mimi, Mbunge wa Kigoma mjini Zito Kabwe na Mheshimiwa Tundu Lisu wa Singida Mashariki tumekubaliana kulivalia njuga suala hili kwa gharama yoyote tunamtaka hai au kama kafa tupewe mifupa yake" Alisema
Alisema kazi ya Usalama wa Taifa ni kuhakikisha Usalama wa nchi upo vizuri na ni lazima watakuwa wanajua haya mambo ya watu kutekwa kwani kazi yao kubwa nikulinda Usalama wa Taifa kwa ujumla.
Lema awashukia TRA Arusha.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo ameitaka Mamlaka ya ukusanyaji wa mapato TRA kuacha kuwanyanyasa wafanyabiashara katika kuwadai kodi kwa kutumia silaha.
Alisema kuna watu wanatumia dhana ya Mkuu wa nchi ya ukali wake kujipatia rushwa kutoka kwa wafanya biashara jambo ambalo amesema rushwa katika ofisi nyingi sasa inaendeshwa kimfumo .
Alisema wafanya biashara kwa sasa wamekuwa waoga kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa watu wa TRA wanaoenda kukagua hadi mauzo kwenye droo za wafanyabiashara hao kwa kutumia maafisa Usalama na takukuru.
" Rais wetu ukali wako na usiriazi wako watu wachini wanautumia vibaya na wanajipatia rushwa kwa kutumia ukali ulionao kwa kuwaogopesha wananchi ili wawape rushwa" alisema.
Hata hivyo Lema alisema Mkoa wa Arusha unaongoza kwa TRA kuwaonea wafanya biashara ambapo alisema yeye kama Mbunge aliyechaguliwa na wananchi atahakikisha anasimamia jambo hilo ili wafanya biashara wasiendelee kunyanyaswa.
Utaratibu wa ukusanyaji mapato hauitaji kutumia njia za bunduki kutishiwa hadi kwenye bar, hapana hili ni jambo la kiungwana unapomfuata mtu kiungwana anakuelewa siyo kutishia kwa kuongozana na Usalama wa Taifa ,askari polisi takukuru na TRA " alisema.
Alisema maduka mengi yamefungwa kutokana na utaratibu mbaya wa kukusanya mapato ambao umekuwa ukiwaogopesha wafanya biashara wengi.
CREDIT: WOINDE SHIZZA
0 maoni:
Post a Comment