Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RC GAMBO:WANANCHI LIPENI KODI ZA MAJENGO ILI KUONDOA USUMBUFU UNAOWEZA KUJITOKEZA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habarimapema  leo ofisini kwake .Picha na Vero Ignatus Blog. Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Pili Mbaruku akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa mkoa  kwa waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus Blog.


Na.Vero Ignatus .Arusha
 
Wananchi wametakiwa kulipa kodi ya majengo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kutokana na Sera ya serikali inayisema kila mwananchi inayomraka takiwa kulipa kodi ya majengo.


Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake na kusema kuwa yapo makundi matatu yanayoaanishwa katika ulipwaji wakodi hizo


Hata hivyo amesema makundi hayo ni Pamoja na wale ambao nyumba zao hazijapimwa wala kufanyiwa tathimini,kundi la pili in wale ambao nyumba zao zimepimwa lakini hazijafanyiwa tathimini kundi la mwisho no wale ambao nyumba zao zimepimwa na kufanyiwa tathimini.


Hata hivyo amesema kundi la kwanza linatakiwa kulipa shilingi elfu 15,000kwa mwaka,ambapo kundi la pili wanatakiwa kulipa waendelee kulipa Kwa utaratibu waliokuwa wanautumia toka awali,kundi la tatu gharama zao zipo juu kulingana na tathimini mpya iliyofanyika mwaka 2015-2016.


Vilevile Gambo ametoa onyo kali Kwa wanasiasa wenye tabia ya kupita Kwa wananchi na kuwapotosha kuhusiana na ulipaji wa kodi hiyo amesema hatua Kali za kisheria zitachukuliwa endapo watambaini mmoja wapo.


Nae meneja wa TRA mkoa wa Arusha Pili Mbaruku amesema kuwa wamejiwekea utaratibu mzuri kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa mitaa ili zoezi la ukusanyaji liwe jepesi kwao badala ya kupanga foleni TRA jambo ambalo litawqchukulia muda wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeza Kwa umoja ili kurahisisha zoezi hilo na kuweza kutekeleza agizo la serikali kulipa kodi
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO