Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UWT YAWAPONGEZA WABUNGE KWA UCHAGUZI, YALAANI KAULI ZA MHE MBOWE

Inline image 1

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unatoa pongezi kwa Wabunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia haki yao  ya kidemokrasia, kikatiba na kikanuni kufanikisha uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 4/4/2017 bungeni mjini Dodoma.

Pia unawapongeza Wabunge waliochaguliwa kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la Afrika Mashariki, tunawataka kuwa wazalendo, waadilifu, wachapakazi
na wenye kutanguliza maslahi ya nchi yetu Tanzania kwanza.

Pia, UWT imeridhishwa na hatua za mchakato wa uchaguzi huo ndani ya Bunge na inapongeza demokrasia pana, komavu na shirikishi iliyooneshwa na wabunge kwa kupiga kura ya HAPANA kwa wagombea waliotokana na CHADEMA kwa sababu uteuzi wao haukuzingatia misingi ya demokrasia, uwakilishi wa Kitaifa wala jinsia.

Uteuzi uliofanywa na CHADEMA hata baada ya kushauriwa, unadhihirisha dharau kubwa na kutothamini mchango wa Wanawake wa Tanzania katika maendeleo ya nchi yetu.


Bunge na Wabunge lazima wawe mstari wa mbele katika juhudi za kuimarisha demokrasia yetu kama Taifa na ndani ya vyama vya siasa, kamwe Bunge lisiruhusu kutumika kama “rubber stamp” kama ambavyo CHADEMA walipanga kwa kuteua wagombea wawili pekee na kwa kufanya hivyo tayari waliamua nani awe mbunge na kulinyima Bunge fursa na uhuru wa kuchagua miongoni
mwa wagombea.

Aidha, UWT imesikitishwa sana na kauli za MATUSI, DHARAU na KEJELI alizozitoa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe dhidi ya Wabunge na Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Kitendo cha Mhe. Mbowe kuwatukana Wabunge sio tu kinakiuka Kanuni za Maadili ya Viongozi lakini pia kinatweza UTU na HESHIMA ya wabunge na bunge mbele ya jamii.

 UWT inaungana na Maamuzi ya Mhe. Spika ya Kuwaita watovu wa nidhamu kwenye Kamati ya Maadili.Hata hivyo tunamtaka Mhe. Freeman Mbowe kuomba radhi wabunge na Umma wa Tanzania kwa lugha isiyo na staha.

Pamoja na kuomba radhi, tunamtaka Mhe Mbowe afute kauli yake ya kuwahusisha na kuwatuhumu Viongozi wa Serikali (Rais na Waziri Mkuu) na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa wameingilia uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ndani ya Bunge.

UWT inaendelea kuwahimiza Wabunge kujadili na kupitisha Bajeti kwa kuzingatia vipaumbele muhimu kwa Maendeleo ya Jamii na Ukuaji wa Uchumi ikiwemo Ujenzi wa Miundombinu ya Maji, Afya, Elimu, Umeme Vijijini, pamoja na kuimarisha njia za Uchukuzi na Mawasiliano k.v Barabara na Reli.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

AMINA MAKILAGI
KATIBU MKUU
UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA {UWT}
05 April, 2017.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO