Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Meya wa Jiji la Arusha Azindua Madarasa ya Shule za Msingi Yaliyokamilika

Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Kalist Lazaro akiambatana na Naibu Meya wa Jiji Mhe. Viola Likindikoki, Diwani wa Kata ya Sinon  na mjumbe wa kamati ya Elimu Mch Simbeli, Afisa Elimu na Afisa Mkaguzi wa Taaluma leo asubuhi wamezindua rasmi madarasa ya shule za msingi yaliyojengwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha mpaka kufikia Aprili 2017.

Uzinduzi huo kwa niaba ya shule zingine umefanyika katika Shule ya Msingi ukombozi Kata ya Sinon.

Mstahiki Meya wa Jiji amewapongeza madiwani wa Kata zenye madarasa hayo na Kamati za Shule kwa kukamilisha ujenzi kwa wakati na ufanisi mkubwa ili kuwawrzesha watoto kupata mahali pa kusomea.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO