Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mashahidi wa kesi ya Uchochezi dhidi ya Ally Bananga Washindwa Kutokea tena Mahakamani

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha Mhe. Msofe ameairisha tena zoezi la kusikiliza mashahidi katika shauri la kesi ya uchochezi inayomkabili Diwani wa Kata ya Sombetini Jijini ArudhaMhe. Ally Bananga hadi Aprili 12 mwaka huu kutona kutokufika kwa mashahidi wa upande wa mashtaka mahakamani hapo hii leo.

Hii ni mara ya pili mashahidi wanashindwa kufika  Mahakamani hapo yangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mfululizo Jumatatu ya wiki hii.

Akizungumzia mwenendo wa kesi hiyo, Wakili wa Mh Bananga, Sheki Mfinanga ameiambia Blogu hii kwamba upande wa mashtaka umeomba kuahirishwa kwa kesi kutokana na shahidi  muhimu (OCID) kuwa na majukumu mengine, jambo ambalo walilipinga kwa niaba ya mteja wake kutokana na ukweli kwamba kina mashahidi wengine ambao wameorodheshwa wangeweza kujitokeza hao. Baadae wakafikiana na Hakimu kuwa hi ni ahirisho la mwisho katika shauri hili.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO