Chama cha Demokarasia na Maendeleo kimafanya uteuzi wa jina la Viola Lazaro Likindikoki kuwa mgombea atakayekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni kujza nafasi ya Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Hatua hiyo ilifikiwa na Kamati Tendaji ya chama hicho Wilaya ya Arusha Mjini siku ya Ijumaa ya tarehe 6 mwezi wa 7 katika Ukumbi wa Safari Hotel baada ya madiwani wa chama hicho kupiga kura.
Katika hatua ya upigaji kura wagombea watatu pekee waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha walichuana vikali na matokeo kuwa Viola Lazaro kura 16, Prosper Remy Msofe kura 9 na Ally Banaga Mwatiga kura 7.
Mshindi na mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya Naibu Meya wa Jiji, Mh Viola Likindikoki akipiga kura |
Diwani wa Moshono Mh Paul Matsen kulia akiteta jambo na Katibu wa CHADEMA Arusha Mjini, Mh Steven Urassa |
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Tendaji ya CHADEMA Arusha Mjini |
Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Mjini, Magoma Jr Magoma akihutubia madiwani (hawaonekani pichani) |
Ally Bananga akitoa nenola shukrani baada ya uchaguzi huo kumalizika namshindi kutangazwa |
Diwani wa Unga Ltd Mh James Lyatuu |
Afisa Uchaguzi wa CHADEMA Arusha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana Innocent Kisanyange |
Mstahiki Meya wJijila Arusha Kalisti Bukhay Lazaro |
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Arusha Mjini Mzee Emmanuale Zakaria (baba Bony) akiteta jambo na Katibu wa BAWACHA Arusha Mjini Happines Charles |
0 maoni:
Post a Comment