Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SIKU YA MABALOZI WA USLALAM BARABARANI ILIVYOFANA MKOANI DODOMA JULAI 8 2017




Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Taifa(Mwenye T-Shirt ya Blue) akiwa ameambatana na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini DCP Mohammed Mpinga ambae pia ni katibu wa Kamati ya usalama barabarani na Mlezi wa RSA Tanzania wakiwa wanaingia uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma baada ya kupokea maandamano ya Mabalozai wa usalama Barabarani yaliyofanyika mapema leo Mjini Dodoma (Makao makuu ya Nchi). Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Mgeni rasmi Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni pamoja na Kamanda wa Usalama barabarani Mohamed Mpinga pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa katika siku ya mabalozi wa usalama barabarani yaliyofanyika katika kiwanja cha mashujaa leo mjini Dodoma .Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus Ignatus
Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni akiwaanazungumza na mabalozi wa usalama barabarani pamoja na wadau mbalimbali ,wageni waalikwa leo mjini Dodoma.Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini DCP Mohammed Mpinga akizungumza katika siku ya mabalozi wa usalama barabarani Mjini Dodoma leo.Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Mkuu wa kitengo cha Elimu nchini Tanzania ASP Mosi Boniface Ndozeikaro akizungumza katika siku ya mabalozi wa usalama barani leo Dodoma .Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus


 Na.Vero Ignatus /Murtadhwa Elbahsan
Siku ya mabalozi wa usalama barabarani (RSA) imefanyika Kitaifa mkoani Dodoma ambapo Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni amekuwa mgeni  rasmi, shughuli hiyo imefanyika katika viwanja vya mashujaa na imewashirikisha mabalozi mbalimbali Tanzania bara na Visiwani.

Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama Taifa John Seka amesea kuwa lengo kuu la siku hiyo ni kuweza kuleta uhamasishaji kwa wananchi  ili waweze kupata elimu ya usalama barabarani na wasione ni jukumu la jeshi la polisi peke yake, kukuza mahusiano na jeshi la polisi  pamoja na mabalozi kufahamiana zaidi na kuwapongeza mabalozi kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya ya kujitolea. 

Kwa upande wake kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani  ambae pia ni katibu wa Baraza la usalama barabarani Taifa DCP  Mohammed Mpinga  amesema kuwa takwimuza vifo na majeruhi zinaonyesha kuwa nchi zinazoendelea zinaathirika sana na tatizo hili hivyo bado tunalo jukumu kubwa la  kupingana na ajali za barabarani 
Ameainisha takwimu za ajali kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017 zimepungua kwa asilimia 44  vifo vimepungua 13% majeruhi 30% ambapo wa asilimia kubwa RSA inahusika kwa kiwango kikubwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi  changamoto  kutambua juhudi za usalama barabarani wanaojitole.

Mpinga ambae  pia ni mlezi wa( RSA)amewapongeza mabalozi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya  kwa kukabiliana na ajali za barabarani kwa kuonya kukaripia pale wanapoana mwenendo mbaya wa madereva pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani
“ Muendelee kujitoa kama vile ambavyo mnavyojitoa  kwani mnalirahisishia kazi jeshi ,mmekuwa mkiokoa maisha ya watu wasife kwa uzembe kwaajali za kujitakia “alisema .

Amezitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na vifaa vya lkutendea kazi,ubovu wa barabara na miundombinu,ukosefu wa alama za barabarani,utashi wa kisiasa ,wadau wanaona suala la usalama barabarani siyo la kwao na haliwahusu.

Mkuu wa kitengo cha Elimu nchini Tanzania ASP Mosi Boniface Ndozero  amesema kuwa mambo mawili lazima yazingatiwe, “ni vyema kuzingatia na kufuata alama za usalama barabarani yote yakizingatiwa ajali  zitapungua kabisa” amesema kuwa jeshi lapolisi nchini kitengo cha elimu limejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa elimu wanayoitoa  inawafikia walengwa pamoja na hayo amesema jeshi la polisi limejipanga  kutoa elimu kwa wanafunzi mashuleni kuhusu elimu ya usalama barabarani 

Kwa upande wake  Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Lazaro Mambosasa  amesema kuwa wanamipango  endelevu  katika mji wa Dodoma  ili ujio wa serikali usije ukaongeza vifo na ajali kwani wamejipanga kuthibiti ajali za barabarani   

Ikumbukwe kuwa RSA imesajiliwa rasmi mwaka 2014 kama taasisi isiyo ya kiserikali ikiwa na wanacham 10 hadi sasa wapo zaidi ya 60,000 kwenye majukwaa ya mitandao wa kijamii (Whatsap, Facebook, Twitter, Instagram nk.), wapo wakurugenzi 8, kanda 5ambazo ni kanda ya kusini, kanda ya kati, kanda ya kaskazini ,kanda ya mashariki,kanda ya ziwa na kanda ya nyanda za juu kusini, wapo maadimini 20 kwenye majukwaa hayo ya mitandao ya kijamii.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Skauti wa mjini Dodoma .Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Mabalozi wa usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja .Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus


Afande Jahnson Kahatano mkurugenzi wa barabara Sumatra Taifa akizungumza kaika siku ya mabalozi wa usalama barabarani.Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
RPC wa mkoa wa Dodoma Afande Mambosasa akizungumza.Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
RTO wa mkoa wa Dodoma Marson Mwakyoma akizungumza.Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Balozi Augustus Fungo akizungumza katika siku ya Mabalozi wa usalama barabarani leo Dodoma .Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Mratibu wa RSA wa kanda ya kati Kelvin John akizungumza.Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Mabalozi wa Usalama barabarani waliovalia tshrit za blue na nyekundu wakiwa katika picha ya pamoja katika siku yao iliyofanyika leo Dodoma .Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Waendesha pikipiki wakiwa katikaa maandaano katika siku ya (RSA DAY)yaliyofanyika mjini Dododma leo.Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus
Waendesha bajaji wakiwa  maandamano hayo leo.



Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO