Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UBORESHAJI BANDARI YA DAR ES SALAAM, ATOA ONYO KWA WANASIASA WAROPOKAJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam katika eneo la Bandari hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.


 Baadhi ya mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakifatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam. 
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kutoa hotuba yake kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird alipokuwa akisoma hotuba yake. 
 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakati wakitazama kipeperushi ya maelezo ya Mradi wa uboreshaji wa Bandari jijini Dar es Salaam. 
 

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.
 
 
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam. 
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine waliosimama wakati Banana Zorro pamoja na Mrisho Mpoto walipokuwa wakiimbawimbo wa Aamka Tufanye kazi kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

WAKATI HUO HUO 
Rais Dk John Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotaka sifa za kisiasa kwa kushabikia waovu hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Rais amesema kuna watu wanashabikia maovu kwa kutoa matamko bila kuyapima madhara yake.

"Niwaombe wanasiasa wanaoshindwa kuzuia midomo yao, wanaosema kuwa hawa watu wameshikiliwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu, katika hali hiyo kwanini usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.Msitufanye tukafika huko"
"Kwanini hata siku moja mtu asijitokeze kulaani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa kutaka sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule...nataka polisi mfanye kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani," amesema Rais John Magufuli na kuongeza;

"Juzi mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa walioagiza hizo uniform za jeshi.

"Endeleeni kujenga heshima ya bandari, rushwa iwe ni marufuku, halafu muda pia... mtu akifika hapa akae muda mfupi na aondoke, hata kama anasafirisha pini ifike inapokwenda na sio ipotelee njiani

"Kuna vichwa 13 vya treni vimeshushwa hapa lakini havijulikani ni vya nani, tena inasemekana ni vibovu na TRL wamesema hawajaagiza na wala hawajasaini mkataba wowote.

"Hamkuuliza vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku nyingine si watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu?
"Sijui haya mavichwa mtafayanyia nini, lakini hili ni lazima lisemwe ili Watanzania wafahamu. Tutangulize uzalendo wa nchi yetu."

PICHA NA IKULU
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO