Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kutoka Ofisi ya RC Gambo: Maonesho ya Kilimo Nane Nane Kufanyika Viwanja vya TASO Njiro Kuanzia Agosti Moja, Mkoa Kuratibu Maandalizi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard  Kwitega amesema kuwa maonyesho ya wakulima maarufu kama nane nane ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja wa Themi Njiro yataendelea kuwepo kama kawaida.
Ameyasema hayo baada yakutokea sitofahamu kwa wananchi kutokana na iliyokuwa taasisi yakusimamia maonyesho hayo (TASO) kuzuiliwa kuendelea kuratibu maonyesho hayo.

Aidha, amesema kwa mwaka huu maonyesho hayo yataratibiwa kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Sekretarieti za Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara pamoja na TASO.
Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ikiwa ndio mwenyeji wa maonyesho hayo ndio imepewa jukumu lakusimamia uwandaaji wa shughuli zote katika viwanja hivyo.

Ametoa wito kwa washiriki wote wa maonyesho hayo kwa mwaka huu  2017 kuanza maandalizi mapema ikiwemo ulipaji wa ada ya ushiriki katika ofisi zilizokuwa za TASO ndani ya viwanja vya nane nane ambapo kwa sasa kuna maafisa walioteuliwa kutoka katika Wizara na Sekretarieti ya Mkoa kutumia ofisi hizo kwa shughuli hizo.

Pia shughuli nyingine za Maandalizi zikiwemo kuwasilisha mahitaji ya idadi ya waoneshaji, Magari, na taarifa nyingine zifanyike katika ofisi za TASO kabla ya Julai 20,2017.

Kwa mwaka huu maonyesho hayo yatabeba kauli mbiu isemayo “Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”,ambayo yataanza rasmi Agosti moja,2017 nakumalizika Agosti 10,2017.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO