Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nyalandu amshukuru Lowassa kuonyesha maisha nje ya CCM



Imeadikwa na Gazeti  Mwananchi
Dar es Salaam. 
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amemtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni, Dar es Salaam kumshukuru “kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM”.
Nyalandu aliyejiondoa CCM wiki iliyopita akidai chama hicho kimekosa mwelekeo, jana alikwenda kujitambulisha kwa mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye alimtangulia kujiunga na chama hicho akitoka CCM wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu 2015.
Mara baada ya Nyalandu kutangaza hatua hiyo wiki iliyopita na kuomba Chadema imfungulie “malango”, harakaharaka Lowassa alimkaribisha na kusema wamelamba dume.
Tangu Lowassa ahamie Chadema akiambatana na baadhi ya wafuasi wake na kugombea urais kupitia chama hicho, amekuwa akisema kuna wafuasi wake wengi waliobaki CCM, lakini hajaweka wazi iwapo Nyalandu ni mmoja wao.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa jana na ofisi binafsi ya Lowassa, ilimnukuu Nyalandu akisema, “Mzee wangu nimekuja kusema asante kutufungulia mlango.”
Baada ya Lowassa kumpokea, picha zilizotolewa na ofisi hiyo ziliwaonyesha wakishikana mkono na kupata kahawa pamoja.
Vilevile taarifa hiyo ilimnukuu Lowassa akimkaribisha Nyalandu katika upinzani na kusema kuwa “Nimefarijika kuja huku, karibu sana tushirikiane na kwa hakika 2020 tutavuka daraja.”
Sababu za kujiuzulu
Akitangaza uamuzi wa kujitoa CCM wiki iliyopita, Nyalandu alisema ni kutokuridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa Watanzania na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi ya mihimili ya dola yaani Serikali, Bunge na Mahakama.
“Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na nafasi zote za uongozi ndani ya chama kuanzia leo Oktoba 30, 2017,” alisema
Nyalandu ambaye hivi karibuni ameonekana kutofautiana na chama chake, ndiye mbunge pekee wa CCM aliyekwenda Nairobi nchini Kenya kumjulia hali mbunge mwenzake wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyejeruhiwa kwa risasi akiwa mjini Dodoma Septemba 7, mwaka huu.
Mbali na hayo, Nyalandu pia alitangaza hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Twitter azma yake ya kupeleka hoja binafsi bungeni ya kutaka mabadiliko ya Katiba, jambo ambalo pia amelitaja kama sababu ya kuondoka CCM.
“Mimi naondoka na kukiacha Chama cha Mapinduzi nikiwa nimekitumia  kuanzia ngazi ya uenyekiti UVCCM ngazi ya mkoa, mjumbe wa kamati za siasa za wilaya, mkoa, mjumbe wa kamati za mkoa na mwisho kabisa nikiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.
“Kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya siasa kiongozi wa kisiasa na kiuchumi, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Nyalandu.
Akifafanua sababu hizo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi, Nyalandu alisema “Chama ni kama mashua au boti iliyokosa mwelekeo ndani ya maji. Hakiendi mashariki, magharibi, kaskazini wala kusini. Na kwa kuwa CCM ndiyo inaongoza Serikali yetu, nikaona huko twendako si sahihi. Nilipoona hivyo nikaamua nihamie upande wa pili.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO