Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)Wafanyika Arusha


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)umefanyika Jijini Arusha tangia kuanzishwa kwake Julai mosi 2015 ambwpo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Kassim Majaliwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Umlemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akifungua mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ukumnbi wa Simba, Kituo cga Mikutano cha Kimataifa, AICC Arusha leo Novemba 29, 2017
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) jijini Arusha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema, katika kipindi kifupi cha miaka miwili tangu WCF ianizshwe Mfuko umeweza kutekeleza wajibu wake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama na kulipa Mafao ya Fidia.

“Mfuko umeanza kufikia wanyonge kwani umeonyesha jinsi ambavyo wafanyakazi wanyonge waliokuwa hawalipwa fidia wanapopata madhara kazini, sasa kutokana na kuwepo kwa Mfuko huu wanyonge wameanza kufaidi matunda kama ambavyo serikali ilidhamiria.

“Nitoe wito kwa viongozi wa Mfuko, endeleeni kutoa elimu kwa wananchi hususan waajiri ili waweze kujisajili na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuwalipa fidia wafanyakazi wao pindi wanapopata madhara wawapo kazini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba amesema hali ya Mfuko ni njema tangu uanzishwe, “Tunapokutana leo hii kwa mara ya kwanza kabisa, napenda kuwajulisha kuwa Mfuko umekuwa ukifanya vizuri katika kuimarika kifedha ambapo kwa mwaka wa kwanza tu, Mfuko ulifikia kiasi cha shilingi Bilioni 65.68 na katika mwaka wake wa pili ambapo ndio huu tulio nao napenda kuwafahamisha kuwa Mfuko umekuwa hadi kufikia Shilingi Bilioni 135 fedha ambazo bado hazijakaguliwa lakini sitarajii tofauti kubwa sana hata zoezi la ukaguzi litakapofanyika”. Amesema Bw. Mshomba.

Aidha Bw. Mshomba alisema, madhumuni ya Mkutano huu wa siku mbili ambao umebeba kauli mbiu ya "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”.  ni kutoa taarifa ya mwaka ya Mfuko, kutathmini maendeleo na changamoto zinazoukabili Mfuko na kupokea maoni ya kuboresha huduma za Mfuko.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba amesema, tangu Mfuko uanzishwe, umetoa mafunzo mbalimbali  kwa wadau wa Mfuko ikiwa ni pamoja na Madaktari.

“Hadi sasa Mfuko umetoa mafunzo kwa Madaktari 504 nchi nzima kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini za ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi”. Amesema Bw. Humba.

Aidha Waziri  ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa mafanikio ambayo Mfuko umeyapata katika kipindi cha muda mfupi tangu uanzishwe.



Kutoka kushoto, Mhe. Waziri Mhagama, Dkt. Irine Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Umlemavu, Mhe. Jenista Mhagama,he. Mhagama na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa.


  
Naibu Waziri wa Nchi Ofiosi ya Waziri Mkuu, Mhe. Anthony Mavunde, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mashomba, akitoa hotuba yake
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri MkuuSera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, wakati alipowasili kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha leo Novemba 29, 2017
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati akiwasili kqwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC jijini Arusha leo Novemba 29, 2017
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na  
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. AbdulsalaamOmar,

 Mbunge wa Chalinze, Mhe., Ridhiwani Kikwete, (kulia), akizungumza na Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Bw. Anslem Peter.
 Afisa wa WCF, Bw. Edward Kirenga, (kushoto), akiwasajili wajumbe wa mkutano


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akitoa hotuba yake.

Dkt. Isaka, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Stella Ikupa, (kushoto), wakati wa mkutano huo.
Kikundi cha bendi ya Mjomba, (Mrisho Mpoto), kikitumbuiza
Viongozi wakishuhudia burudani ya kikundi cha bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto.
Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Bw.Anselim Peter, (wapili kulia), akijadiliana jambo na maafisa wa Mfuko huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Dkt. Irine Isaka, (kulia), akisalimiana na Meneja Mafao wa WCF, Bi. Rehema Kabongo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), Meshac Bandawe , (kushoto), akisalim iana na Meneje Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele
Wajumbe wamkien delea kusajiliwa kabla ya kuingia ukumbini.
Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Emmnuel Humba, (kulia), akibadilishana mawazo na wajumbe wenzake wa bodi, Dkt. Francis Michael, (wapili kulia), na Bw.Richard Wambali

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO